Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Watu wakisema hawataki kuoa wana maanisha unapika mpaka wali wa nazi noma yaani [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mdogo mdogo, nimetoka kuvuta mzigo huo, wa Seapiano ... Kwahyo nitakuwa huru, kwenye ulaji wa mbususu.. bira majirani kusikia sauti za mliwaji..
IMG_20220525_193325.jpg


Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Ghetto ninaloishi lina mkeka,ndoo ya maji na mifuko yangu ya nguo..napambana nafanya biashara ya kutembeza bidhaa za urembo.wiki hii mambo ni mazuri jumatatu mauzo yalikuwa 37,000 leo 26,000 napambana kutafuta hela pia nasali sana ili mwaka 2023 nije kuwa na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani..

Matumizi yangu hayafiki 5000 kwa siku na mara nyingi ni chini ya 4000 hela ya kula naitoa kwenye biashara hii hii ambayo niliianza jumatano iliyopita hadi jumapili nilipumzika niweza kusave 63,000 hadi leo na nimeshatoa hela ya kwenda kuongeza vitu kesho kariakoo..

Lengo langu niongeze biashara ya pembeni ili inigharamie bill zangu za kila siku.Lengo langu la mwaka ujao niwe na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani vilevile ninunue bodaboda hata ya mtumba iniingizie pesa na vilevile niwekeze kwenye kilimo kama sitafanikiwa katika yote hayo matatu basi at least hayo malengo mawili yatimie.

Uzi huu umenigusa sana hadi nmeamua kuishi mwenyewe kwangu kiukweli sijawahi kuandika post ndefu kuliko hii hapa JF ila kwa hisani ya uzi huu nimeshare jambo langu smartphone yenyewe ninayotumia ni majanga panapo majaaliwa nitaleta mrejesho wa maendeleo ya biashara na picha ghetto langu kwa sasa..

Roger that!
all the best masta
 
Maisha ya geto, ugali mkubwaa dagaa wa kuhesabu.. aisee dagaa wana save sana budget , pale unapokuwa umefuria... View attachment 2215300
Daaah umenitama isha mzee huu ndio msosi wangu pendwa huwa jasho lazima linitokea.

Huwa nahakikisha dagaa zinatoka tamu ile mbaya

Ingridient zangu

Dagaa

Pilipili huwa nasagia kwenye nyanya na brenda.

Kitunguu maji

Kitunguu swaumu

Tangawizi

Chumvi

Mafuta.

Daaah ngoja leo nipige hii kitu nimemiss sana.[emoji2][emoji1787][emoji39]
 
Nlipost hiii mwaka 2020 na badae December mwaka huo huo nikawa nasepa maskan kwenda kuanza maisha kitaaa bila kuwa na mishe yoyote. Kiukweli nilipiga kazi yoyote iliokuja mbele yangu na hiii ikansaidia kukutana na washikaj mbalimbali ambao ikasaidia kupeana michongo. Hadi Sasa npo get naona hatua zinaenda ila kwa mwendo wa Kobe.
Kikubwa usirudi songa mbele
 
Wajuba mko vizuri..mi kwenye kuosha vyombo na kupika,naonaga ishu kichizi yan
Ukitaka usiwe mvivu wa kuosha vyombo baada ya kupika fanya hivi ÷

Kwanza; usiwe na vyombo vingi ghetto, uwe na vichache vya muhimu tu.

Pili; ukiwa unapika kila chombo ambacho hakina matumizi baada ya kumaliza kazi yake hakikisha unakiosha au unakisuuza na kuirudisha mahali pake.

Mpaka unamaliza kupika utajikuta huna chombo hata kimoja kichafu isipokuwa ulivyopikia na utakavyotumia wakati wa kula. Hivi haviwezi kukutia uvivu kuosha maana ni vichache.

Kwanini nasema uwe na vyombo vichache, kwanza siyo hulka mwanaume ghetto kwake kuwe na vyombo vingi vya kupikia hii ni kazi ya wanawake.

Ukiwa na vyombo vingi vitakufanya uwe unatumia tumia tu maana unavyo vingi na unaona uvivu wa kuosho vichafu.

Sasa hii itakukusanyia vyombo vingi vichafu na vitakutia uvivu wa kuosha na hutapika, bajeti yako utaivuruga kwenda kula nje wakati kila kitu unacho ndani.

Wengine husema kwa kuwa yupo dada wa jirani au mwenye nyumba nitamuita aje anioshee, kosa la kiufundi hapa unafanya. Utaoa/kuozeshwa kabla ya muda wako.

Kuoa/kuolewa huwa siyo umri bali ni utayari wa mtu kwamba anaingia kwenye majukumu haya. Usiige kila mtu ana akili zake jinsi ya kuishi kwenye ndoa.

Kuna vijana tulianza wote maisha wakawahi kuoa, mwaka juzi nakutana nao wanasema bora wasingeoa mapema wanasema angalau sasa hivi ndio wangeoa ili wawe wamejijenga zaidi kimaisha.

Wanaume wengi huamua kuoa mapema baada ya kuchoshwa na kuosha vyombo na kupika, Tumia hiyo njia kwanza,chakula cha kujipikia ni bora na ni afya zaidi kuliko cha nje.
 
Back
Top Bottom