Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Wakuu nina mengi ya kusimulia jamvini ttzo mwandiko mbovu,, nitaeleza Kwa kufupisha,,,,
Ukiamini Mungu na kuishi kwa Imani huku ukijituma Kwa nguv zote baraka utaziona.

Nilipo yaanza maisha rasimi baada ya kumaliza masomo yangu, safari yangu ilianzia Dodoma, sina ndugu nilifikia Kwa Wana walionitangulia kumaliza nashkuru walinipokea vzr tukaishi japokuwa baadhi ya changamoto nilipitia zisizo na maumivu kwani nilikua napata wakt mgumu pale mwana akija demu wake kitu ambacho kilitia uchachu wa kufight nikapange kwangu.

Nilitoka mbali na home wazaz wakiwa hawataki ila vile nilkua nishajiapia baada ya kumaliza chuo lazima nitoke mbali na home Kwa ajili ya kutafuta maisha,, nilifanya kama nilivyojipangia tangu nasoma,, wakati nakalibia kumaliza chuo miezi ya mwishoni mpenz wangu alibeba ujauzito wangu ikawa mkazo wa me kuwa mbali.
Mama mtu akabless me kutoka Kwa ajili ya kutafuta ili tuje tuishi wote. Nimeseto Kwa Wana Kwa miez 4 muda huo najitafuta katika ofsi flan hapa dodoma.
Mpka Sasa naandika ushuhuda huu nipo kwangu nilipo panga naishi na Mke wangu pamoja na mtoto wetu, life liko good kiasi Kila hitaji tunapata, kwa uweza wa M/Mungu mwakani tunahamia kwetu.
Nilicho jifunza kwenye maisha usiogope mtangulize Mungu katika kila jambo lako fanya kazi Kwa bidii mmbo yanajipa yenyewe,,,, zingatio Kwa sisi vijana wanawake Wana nguvu kubwa sana haswa ukimpata ambaye anajielewa na aliyetayari kufanya maisha katika kila hali.

Vilivyo Anza mpaka now,,, vijana tusikate tamaa Mungu sio wa kabila moja. View attachment 2389183View attachment 2389186View attachment 2389196View attachment 2389197View attachment 2389199View attachment 2389204
Big Up sana Mkuu
 
Kama demu anaeleweka, basi utafanya mengi ya maendeleo ndani ya muda mfupi.

Nilivyoamuaga kupanga, soon nikaanza kuishi na mwanamke. Nilikuwa nikipata 300k, yeye nampa 250k, alaf namwambia hii ndio ipo, utaplan ufanyie Nini, lakini utakachofanyia naomba uniambie.

Nilinotice mle ndani vitu vikaanza kuongezeka mdogo mdogo, mara vyombo, sufuria, rice cooker, pressure cooker etc. Kuna kipindi nikamwambia nataka tuanze kudunduliza tununue Tv na king'amuzi. Budget yangu kwenye Tv ilikuwa 400k kwa inch 32. Hiyo siku nikampa 200k, aitunze ili next month nijazie ikamilike na king'amuzi, hakupokea Ile hela, akaniambia subiria, akaenda kupekua pekua kwenye nguo zake akanja na 700k (kumbe alikuwa anawekaga akiba), plus Ile 200k tukawa na 900k, akaniambia kanunue Tv kubwa, next month ndo tutabuy king'amuzi. I was surprised, sikuexpect that.

After that day, kuna siku tunachek tamthilia after kula, akaniambia Kodi hii ikiisha, tukalipia tena itakuwa mara ya mwisho kukaa hapa, inabidi tuhamie sehem yenye chumba na sebule. Nikamuuliza tutaweza kumudu gharama za chumba na sebule? Akanijibu Kila kitu kinawezekena tukijipanga, ndio maana nimekushirikisha mapema. Na kweli, after a while, tukahamia sehemu nyingine.

Hata ikitokea mishe zimekuwa tight kiasi gani, kahela kadogo ninakokapata huwa namkabidhi yeye asimamie matumizi yake, kwa upande wangu Niko very careless na hela, uwepo wake umenifanya ni accomplish vitu vingi ndani ya muda mchache, ambavyo peke yangu nisingeweza maana Hela yangu nyingi ilikuwa inapotelea kwa muhindi (betting).

Sina mchongo wa maana hapa Mjini, lakini friji Iko full, mchele, unga na mboga mboga zipo, kiasi kwamba hata nikisota mwezi, tunauhakika wa kula na kulala sehemu nzuri. Washkaji zangu wakijaga kunitembelea huwaga hawaamini wanachokiona.

So, back to the topic mkuu Secret ID kama huyo manzi anaeleweka, jilipue tu, haya maisha tunayoishi Kila kitu tunachofanya ni tunabet, results zitajishow mbeleni.
Kaka unamke hapo
 
Wadau naombeni kufahamishwa jinsi kutumia Smart TV upande wa internet ya kwaida siyo Wi-fi
Kwa ninavyofahamu zinakuwaga na Ethernet port so unaweza tumia hiyo kwa kutumia Ethernet cable kuunganisha na router! Mwenye ujuzi zaidi aongeze!!
 
Enzi hizo
IMG_20200901_194939_683_transcpr.jpg
 
Waliowahi kuishi nyumba ya kupanga ambayo wapangaji wote mnashare mlango mkubwa wa kuingia na kutokea ,kero zipi mlipitia kabla hatujitosa ,tupeni Muongozo!!
 
Back
Top Bottom