Kama demu anaeleweka, basi utafanya mengi ya maendeleo ndani ya muda mfupi.
Nilivyoamuaga kupanga, soon nikaanza kuishi na mwanamke. Nilikuwa nikipata 300k, yeye nampa 250k, alaf namwambia hii ndio ipo, utaplan ufanyie Nini, lakini utakachofanyia naomba uniambie.
Nilinotice mle ndani vitu vikaanza kuongezeka mdogo mdogo, mara vyombo, sufuria, rice cooker, pressure cooker etc. Kuna kipindi nikamwambia nataka tuanze kudunduliza tununue Tv na king'amuzi. Budget yangu kwenye Tv ilikuwa 400k kwa inch 32. Hiyo siku nikampa 200k, aitunze ili next month nijazie ikamilike na king'amuzi, hakupokea Ile hela, akaniambia subiria, akaenda kupekua pekua kwenye nguo zake akanja na 700k (kumbe alikuwa anawekaga akiba), plus Ile 200k tukawa na 900k, akaniambia kanunue Tv kubwa, next month ndo tutabuy king'amuzi. I was surprised, sikuexpect that.
After that day, kuna siku tunachek tamthilia after kula, akaniambia Kodi hii ikiisha, tukalipia tena itakuwa mara ya mwisho kukaa hapa, inabidi tuhamie sehem yenye chumba na sebule. Nikamuuliza tutaweza kumudu gharama za chumba na sebule? Akanijibu Kila kitu kinawezekena tukijipanga, ndio maana nimekushirikisha mapema. Na kweli, after a while, tukahamia sehemu nyingine.
Hata ikitokea mishe zimekuwa tight kiasi gani, kahela kadogo ninakokapata huwa namkabidhi yeye asimamie matumizi yake, kwa upande wangu Niko very careless na hela, uwepo wake umenifanya ni accomplish vitu vingi ndani ya muda mchache, ambavyo peke yangu nisingeweza maana Hela yangu nyingi ilikuwa inapotelea kwa muhindi (betting).
Sina mchongo wa maana hapa Mjini, lakini friji Iko full, mchele, unga na mboga mboga zipo, kiasi kwamba hata nikisota mwezi, tunauhakika wa kula na kulala sehemu nzuri. Washkaji zangu wakijaga kunitembelea huwaga hawaamini wanachokiona.
So, back to the topic mkuu
Secret ID kama huyo manzi anaeleweka, jilipue tu, haya maisha tunayoishi Kila kitu tunachofanya ni tunabet, results zitajishow mbeleni.