Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Wadau wa ghetto hamjambo? Mimi nilianza maisha ya ghetto mwezi wa 5 mwaka huu.Naishi maeneo ya uswahilini sana.Sasa jana wakati narudi kutoka kwenye mishe zangu nikakuta nimeibiwa hela.Ni shilingi elfu hamsini tu, kiukweli ni hela ndogo sana lakini ninavyoipata kwa shida inasababisha iniume kwa kweli.Kitu kibaya zaidi wakati naanza maisha ya ghetto bi mkubwa alinionya sana kuweka hela cash chumbani nilipopanga .
Kuweka hela ndogondogo kwenye simu naona ni usumbufu haswa pale inapokatwa wakati wa kutoa. Inaniuma sana yani nimeingia kanisani huku nina kinyongo.
Muwe na Jumapili njema.
Nikuoe namba za wataalam
 
Mi Adamu, Hawa ndio alienishawishi kula tunda la mti wa Kati.
 
Sentensi yako ya mwisho nimeipenda sana.
Kabisa Mkuu, ghetto ni mahala pa kuheshimika, ghetto ndipo unaporudi kupumzisha akili na mwili ukitoka kuzisaka so sio poa kulaza laza kila mtu. Wahuni wanasema,baraka huanzia mahala unapoamkia (Ghetto), so tupunguze hizi ingiz toka ili kulinda BLESSINGS za ghetto.[emoji109][emoji109][emoji109]

NB:
Inafariji sana kurudi na buku 3 kwako(ghetto) kuliko kurudi na laki moja kwa shemeji yako.
 
Kukaa veto sio ngumu sana kiivo huwa ni maaamuzi yanayoshabiiana na ndoto za kujitegemea, ndoto za uraji huru ,ndoto za kutengeneza familia, ndoto za kazi binafsi ,ndoto zakupambana dhidi ya umaskini tegemezi, hiii ya kupanga geto wanetu wanaita kuchomoka kwa maza mi naiita kujitegemea kifikra na ndio mana ni ndoto na geto ni ndoto tu ukishajitegemea ukakosa chakula utaota mandoto tu[emoji23]
Mashallah mtoto wa kiume mrembo
 
Dah wakubwa niaje aisee ...? Leo nalala gheto kwa mara ya kwanza tangu nlivorudsha mpira kwa kipa mwaka jana mweZi wa 3...nmejipanga sio kitoto kama mandonga vile godoro jipya kitanda kipya home theatre ndoo zangu 3 napeta nadhani had mwezi wa 3 mwakAni mungu akibariki ntajibless na flat....wengine ambao bado wanafosi mungu awasaidie [emoji120][emoji120]
Safi sana bishoo[emoji109][emoji109]
 
Back
Top Bottom