Dah,umenikumbusha mbalii.
Nilipendwa na mtoto wa headmaster wetu,binti sijui kilimvutia nini kwangu kwakweli maana kamenisumbua sana,nimekula Chocolate balaa, biscuit naletewa Yale makopo,mpaka na msosi wa nyumbani kwao najilia kama boss.
Chakula cha shule nilikisahau kwa muda,mtoto alikolea na mimi akawa haambiwi asikii. Kulikuwa na kiongozi wa chakula anamuelewa sanaa binti,na amewekeza pocket money yake kwa binti,Ila mchuchu hajamuelewa mwamba hata kidogo.
Jamaa katuma sana zawadii, nyingine zinarudishwa lakini mwamba anakomaa tu,ikabidi jamaa aanze kuchunguza nani anamzidi kete kwa binti?
Kwenye fukunyua fukunya yake akazipata kuwa binti anamuelewa sana flanii mpaka zawadii anampelekea,na msosi wa nyumbani analetewa,weeeh!!
Balaa lilianzia hapo,ubaya sikuwa na status yoyote school,nikaanza kupewa vikesi vya ajabu ajabu, wakati huo sijashtukia mchongo kwamba kuna mtu anateseka na mimi.
Siku hiyo tulipewa kazi ya kupakua magunia ya mahindi kutoa stoo tupeleke mashineni,na nilipewa kazi ya kusimamia Ile shughuli.
Jioni nashangaa nafuatwa prepo na kiranja mkuu,unahitajika office ya mwalimu wa nidhamu. Tukaongozana,mara anauliza lile gunia uliloiba umelificha wapi,nikabaki mdomo wazi,kuiba gunia tenaa?
Kufika mwalimu akanimbia nina kesi ya wizi inanikabili,kama sitaki matatizo nihakikishe gunia linapatikana. Nikamwambia sina la kujitetea maana sijaiba,nasubiri hukumu,akang'aka balaa kumbe we kiburiii,badala uombe msamahaa unajifanya mjuaji,nikamwambia ticha sijawahi kuiba na sitarajii kuwa mwizi, kwahiyo usinilazimishe kuomba msamaha kwa jambo ambalo sijatenda,akanifukuza ofisini kwake akanimbia tutaona Kesho na ujuaji wako.
Mzuka wa kusoma ukakata,nikawaza hii imekuwajee,mimi huyuhuyuuu niibe gunia nalitoaje nje wakati shule inauzio?
HUKUMU.
Asubuhi kumekucha,ikapigwa kengele,tukakusanyika wote. Nikaitwa mbele na kusomewa hukumu yangu,kwamba mimi ni mwizi nimeiba gunia kwa kushilikiana na mpeshi,hivyo nikafurushwa wiki mbili nirudi na mzazi na mpishi akaachishwa kazi.
Kilichomkuta jamaa baada ya kujua katengeneza mchongo,hata sahau maishaa.
Ila mtoto wa headmaster sitamsahau,ilinipa ufalme kwenye milki ya Baba yake.