Ulifanya kosa gani Shuleni Hadi kengele ya dharura ikagongwa watu wakaja mstarini kwa ajili yako?

Hapa ni katika level zote 3 za elimu shule ya Msingi, sekondari na Kidato cha 5 na cha 6.

Mimi nakumbuka niliwahi kamatwa na simu kengele ikagongwa nikaipasua kwa mawe hadharani..
kama ulisoma shule pote ulikopita na hujawahi kugongewa kengele ya dharura basi wewe ulikuw kondoo hukuwa unajiongeza
 
nilikua nauza mzizi wa kuongeza nguvu za kiume maarufu kama MKONGORA. nilikutwa na hiyo mizizi mfuko mzima ule wa kubebea madaftari ulioandikwa SPORT wenye kamba unavaa kama X hivi. kengele ikagongwa nikapata bakora km 20 na ushee, sitasahau! shule nilikuwa naitwa TIPPU TIPPU kwasababu ya biashara ya MKONGORA.
 
Mi dingi yangu alikuwa boss wa waalimu wilaya fulani early 1990's na alikuwa kauzu sana,nilizingua nyumbani wakati nipo darasa la nne,akaja shuleni bila taarifa yoyote akagonga kengere mwenyewe, wanafunzi wote mstarini,mi sina hili wala lile nikajua mshua amekuja na mishe zake za Kazi, daah si nikaitwa mbele ya wanafunzi kama 400 hivi,dingi akaomba fimbo,nikala fimbo tano,baada ya hapo akasema makosa yangu na kutoa wosia pale,basi tukarudi darasani,nilichukia sana.

NB: Pamoja na hayo lakini Baba alikuwa mtu poa sana,ukipigana huko umepiga mtoto wa mtu,pale kwenye kesi atakuwa mkali sana ila mkitoka anakwambia safi,usikubali kuonewa kizembe,mengi aliyonihimiza yamekuwa msaada mkubwa sana kwenye maisha yangu.REST IN PEACE (25/11/1998)
 
Niligombea u_headboy nikashindwa Ila wakati wa kutangaza matokeo nikayakataa mbele ya walimu na watumishi wa shule kwa kelele ,wale wanaonikubali nao wakazifuata kelele zangu .
Nikala fimbo nikapoa ,usiku nikashika mic ya chapple wakati kimetulia watu wapo kujisomea nikawatangazia kuwa Mimi ndiye head boy wa shule na aliyepita hatambuliki na yeyote .

Watu wakapiga kelele za shangwe ,asubuhi kengele ikagongwa nikala suspension ya miezi miwili na faini ya milioni mbili kwa kuvunja viti vya chapple maana wafuasi wangu walifanya fujo wakati najitangaza hivyo waliharibu Mali za chapple .

Nimerudi kutoka kutumikia kifungo nikapewa uongozi wa nidhamu ni hapo nikatulia na kuanza kuwasaliti wanafunzi wenzangu wasaliti japo nao walinikunguta walipoona nimebadilika kabisa .

Hivyo naamini hamna kitu kikubwa Kama kucheza na psychology ya mtu ,maticha walijua kucheza na akili yangu Ila wakaniponza school mob ikataka kuniua .😀😀
 
Kutega vioo chini kwenye sakafu ili nichungulie chupi za Mademu.
Kioo Cha Kwanza si akaja kusimama Mwalimu bila kujua.

Tukaona mzigo umevimbiana, Wana wakacheka Sana wakashindwa kujizuia.
Mwalimu hakuelewa Hadi baadae alipo pelekewa udaku na wahanga wenzie.

Kiliwaka eenh.
 
Niligombea u_headboy nikashindwa Ila wakati wa kutangaza matokeo nikayakataa mbele ya walimu na watumishi wa shule kwa kelele ,wale wanaonikubali nao wakazifuata kelele zangu .
Nikala fimbo nikapoa ,usiku nikashika mic ya chapple wakati kimetulia watu wapo kujisomea nikawatangazia kuwa Mimi ndiye head boy wa shule na aliyepita hatambuliki na yeyote .

Watu wakapiga kelele za shangwe ,asubuhi kengele ikagongwa nikala suspension ya miezi miwili na faini ya milioni mbili kwa kuvunja viti vya chapple maana wafuasi wangu walifanya fujo wakati najitangaza hivyo waliharibu Mali za chapple .

Nimerudi kutoka kutumikia kifungo nikapewa uongozi wa nidhamu ni hapo nikatulia na kuanza kuwasaliti wanafunzi wenzangu wasaliti japo nao walinikunguta walipoona nimebadilika kabisa .

Hivyo naamini hamna kitu kikubwa Kama kucheza na psychology ya mtu ,maticha walijua kucheza na akili yangu Ila wakaniponza school mob ikataka kuniua .😀😀
Kishule shule Lazima ulipewa jina la Snitch.
 
nilichongesha muhuri washule,nikafanyia mazoezi sahihi ya basa nikapatia ,nikaenda mjini kufanikisha kitabu Cha risiti , masela wakaanza kulipa ada na michango kwangu........ mpaka Leo shule ilikula hasara Milion of money,kumbe kwenye masela palikuwa na kenge ,akashindwa kujitetea lakini hakunitaja mpaka Leo na meja jeshi la goma congo

ebwana ,Ile siku siisahau mana nilitakiwa nitajwe ila hakunitaja
Mpaka Leo ,pamoja Yuko jeshi la kongo Mimi ndo mshauri binafsi
 
Ulitisha Sana komredi
 
Back
Top Bottom