Ulifanya kosa gani Shuleni Hadi kengele ya dharura ikagongwa watu wakaja mstarini kwa ajili yako?

Hapa ni katika level zote 3 za elimu shule ya Msingi, sekondari na Kidato cha 5 na cha 6.

Mimi nakumbuka niliwahi kamatwa na simu kengele ikagongwa nikaipasua kwa mawe hadharani..
Nili kata nywele za binti wa kihindi tukaitishwa wote kuambiwa nimekua suspended mpaka nitakapo resolve issue angu na familia ya binti.
 
nyanda za juu kusini Tena shule maarufu ,kwangu walikaa chini na kwa umri wangu nimepewa kipaumbele kuwa mlezi wa shule......na nimekuwa kipaumbele hakuna kupokea karo mkononi mzazi aingize akaunti ya shule
Hatari na nusu.
 
Hahaha. Snitch kacheki ngono na bado kawasnitch shubamiit.
 
Wewe ulibusu Nyuki🤣🤣🤣Kwa mudomo
 
Wewe ulibusu Nyuki🤣🤣🤣Kwa mudomo
 
Hahaaa!!!

Nilisomaga shule moja ya kulipia, ile shule ilikua primary & secondary. (Zote boarding)

Primary walikua wanalipa ada za maana, hata msosi wao ulikua wa maana, mixer mikate na blueband, chai ya maziwa, mayai etc,

Sie wa secondary ada ilikua kawaida tu, so hata huduma zetu ni kawaida kama kayumba tu lakini wote tulikua compound moja na shule zote mmiliki ni mmoja.

Na kama unavyojua shule za boarding kitengo cha misosi, kila siku ni ugali mchana, ugali usiku, mboga ni maharagwe mwanzo mwenga. Wali ilikua ni alhamis mchana(ukikosa hapo ni mpaka next week )

Nilikua na kampani ya washkaji zangu, jumla tulikua wanne, kama masihara sijui ata tulianzaje tukawa na mchezo wa kuzamia jiko la primary, tunaiba maandazi na maziwa.

Ikifika usiku(mida ya prepo) sie tunachomoka mmoja mmoja darasani tena kwa ishara, tunaenda kukutana kwa mkapa(jikoni)

Kuna kidirisha kidogo wanachotumia kugawia msosi, sasa kile kidirisha kilikua hakifungi, kinarudishiwa tu(ni vile vya nondo)

Sie ndio tukawa tunapenya pale tunaingia jikoni, tunakuuuula maandazi weee na kunywa maziwa kama mapanya, then hao tunarudi darasani tukiwa tunafuta midomo tu, huku tunawacheka kisiri siri wenzetu waliokula ugali maharagwe.

Mwanzo ilikua wanazama watatu, mmoja anabaki akisoma ramani, kuangalia kama mlinzi anakuja ama la, so mkitoka mnamletea na yeye maandazi na ikitokea mlinzi anakuja, jamaa anawastua mnajikausha mle jikoni kimyaaa, mlinzi akija anapita pita tu then anaondoka nyie mnaanza mashambulizi upya.

Baada ya kuzoea mchezo ule ikaja kuonekana kwamba mtu anaebaki nje kuangalia soo, hafaidi vizuri, maana mkitoka mnamletea maandazi tu, maziwa hapati, hivyo tukaamua kuwa kila mtu ni lazima azamie(hakuna cha kubaki kucheki soo) Mistake no 1

Tulivyokubuhu na mchezo ule, tukaanza kuzamia na mabegi na chupa. Tukiingia ni uharibifu wa maana.

Maandazi yalikua yanawekwa kwenye ndoo, kwa hiyo ukizama ndani, unafungua zipu ya begi lako kisha unalivalisha kwenye mdomo wa ndoo, kisha unanyanyua juu chini(kama wnavyofanya wauza nyanya na vitunguu kwenye visado njiani), mzigo wooote unaingia kwenye begi, maziwa mnamimina kwenye chupa, then haoooo mnasepa. Ilifika point kuna mshkaji wa nje alikua anakuja kununua maandazi kwetu na yeye anaenda kuuza.

Mie binafsi ilikua nikiingia cha kwanza napiga vikombe viwili vya maziwa fresh bariiidiiii (kupoza koo)kisha ndio naanza mashambulizi.

Siku hiyo kumbe kuna mtego umewekwa bwana, tumezama vizuuri tu, mie kama kawaida huyooo kwenye vikombe 🍵 nikachukua kimoja kisha huyoo kwenye friji(ni giza lakini ramani yooote naijua) nimepiga funda la kwanza fresh ile napiga la pili nashangaa mwanga mkali balaa unanimulika usoni (I was like am I dreaming!!!??? red handed na kikombe cha maziwa tena jiko la primary daaah) tochi nne zinamulika from different angles.

Ndo ikawa hivyo tena, kengele ikagongwa usiku ule ule(9:30pm) wanafunzi woote shule nzima wakaambiwa wanatakiwa kwenda eneo la jikoni kuna dharula, kufika jikoni wanatukuta wazee wa kazi tupo ndani ya jiko.

Shule nzima mwanangu wanatuzomea tu, halafu nilikua nina penzi jipya na kishombe shombe flani so ilikua noma sana yani.

Wale washenz walisubiri shule nzima imefika ndio wakatutoa mle jikoni.

Ila mwisho wa siku maisha mengine yaliendelea.
 
Ukitengeneza Imaginary picture lazima ucheke mlikamatwa kama wagoni
 

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nimecheka kisenge
 
Kama wewe sio tajiri mpaka muda huu utakuwa ni msengyee kinyama Mana una akili za utafutaji. Nitafute ule bia na nyyama mpaka uzikimbie. Huwa nazikubali hizi akili. Inatakiwa mtu ana hack bank accounts anachomoa hela
 
Wewe jamaa wewe kutoka mikoa ya Mara au Mwanza ulitisha,hata kujiridhisha tu kuwa madame yupo hakuna?
 
Nilikuwa na kawaida ya kwenda jikoni kupakua chakula iwe ugali au wali na maharage na weka kwenye ndoo ya lita kumi halafu natokomea porini kwenda kula nikishiba nafata masela wanakuja kumaliza mchezo.

Siku ya kukamatwa nilifika porini kama kawaida niakenda kunya kwanza ili nije nile vizuri kabisa bila shida yoyote ile
Kumbe second siku hiyo alikuwa anatafuta beberu lake la mbuzi lilifungulia kwenye kamba nakutokomea huko porini.

Kama ndoto vile mara huyu hapa yeye mwenyewe alishituka kwanza. Mara akaniambia nawewe umetoa wapi hiki chakula? sikuwa na na neno alipokiangalia akagundua ni hapo skull moja kwa moja akaniambia tangulia shuleni

Tukapita jikoni yule mpishi akaulizwa akasema hajui chochote sema ukweli alikuwa rafiki yangu aliogopa kurinda kibarua chake. Hadi pared tukafika kengele ikangogwa saa8 hiyo. Ilikuwa aibu sana nikaambiwa nile nikimalize nisipomaliza ndo viboko vitahusika nikaletewa kiti na maji ya kunywa nikaanza ila sikumaliza.

kama kuna mdau yumo humu na anakumbuka hili tukio basi ni mimi we taja shule tu ya kanda ya ziwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…