Ulifanya kosa gani Shuleni Hadi kengele ya dharura ikagongwa watu wakaja mstarini kwa ajili yako?

Kuna siku moja tukiwa tunarejea nyumbani baada ya masomo kipindi hicho nipo O-level, ulikuwa msimu wa mahindi bado mwezi kama mmoja kuanza kukomaa. Njia tuliyopita ilikuwaa na mashamba mengi ya mahindi, rafiki zangu watatu walisogelea shamba na kuvunja mihindi kwa ajili ya migagi (ina radha kama miwa kwa mbali), baada ya hapo mimi kama mla doria nikawa nawapa ishara, baada ya dakika kama mbili hivi walitoka jamaa wawili wanakimbia kutoka upande wa ndani wa shamba wanawafuata wadau waliokuwa wanavunja mahindi.

Ili kuepuka kesi mimi na jamaa mmoja ambaye alikuwa ameshika mabegi ya rafiki zetu waliozama ndani wala hatukukimbia tulikaa kimya tu. Jamaa wale wawili walikuwa wanachomoka kama mshale kuwasaka wale wash' kaji zetu.

Baada ya kukimbizana kwa muda mrefu walifanikiwa kuwakaribia na kuwakalili majina yao kwakuwa walikuwa wakikaa nao mtaa mmoja.

Fast forward Jumatatu imefika majira ya mapumziko iligongwa Kengele wote tukaitwa Assembly ground. Nilipoangalia mbele namuona mwalimu wa nidhamu, jamaa fulani mkaksi levo ya mwisho. Huyu alikuwa akifahamika kwa jina la Mboya, mtaalamu wa Geography.

Wale jamaa waliokaririwa majina yao waliitwa mbele, ghafla waliokuja kushtaki wakadai walikuwepo na watu wengine. Mwalimu akawaruhusu jamaa waje kufanya scanning mstari kwa mstari, hio ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwa kama James Bond, alikuwa akienda mbele narudi nyuma akianza kuangalia nyuma naanza kufunga kamba za viatu 😂😂😂

Baada ya kutokuniona mimi na yule jamaa mbeba mabegi ambaye alikimbilia chooni mwamba alirejea mbele na kuanza kuangaza.

Jamaa zetu walibebeshwa mahindi yote ambayo yalikuwa ya.evunjwa kule shambani. Tulikuja kujua kwamba lile lilikuwa shamba la kanisa, na hao jamaa waliokuwa wakikimbiza rafiki zetu ndio waliokuwa walinzi wa shamba.
 
🤣🤣🤣
 
Hapa ni katika level zote 3 za elimu shule ya Msingi, sekondari na Kidato cha 5 na cha 6.

Mimi nakumbuka niliwahi kamatwa na simu kengele ikagongwa nikaipasua kwa mawe hadharani..
Mimi nilikuwa najulikana najua sana kuchora, sasa kuna siku ikakamatwa picha ya kuchora ya mwanamke yupo uchi, na hapo tupo darasa la tano tu, watu kubanwa kuulizwa wote kimya, ila monitress kubanwa anasema atakuwa incharge tu maana ndio anajua kuchora hapa darasani, aise nilitandikwa nikapelekwa chumba cha walimu nikawa nimepigishwa magoti,
Kila mwalimu akiingia anauliza huyu nae vipi aakionyeshwa ile picha tu na yeye ananimalizia hasira zake.
Ikaitwa assembly nikaja kuokolewa na mdosi mmoja demu, akasema sio huyu nilimuona ahmed wakati anachora ndio ikawa pona yangu, yule muarabu ahmed akafukuzwa shule aise
 
Mzee alitisha sana
 
Mimi nilisuka barua Kali sana ya Mapenzi nikiwa darasa la nne kwenda kwa Binti Moja wa mondo B. Ee bwana ee! Kwanini alitimbe nalo ofisini kwa Maasai Moja mwenye masifa sana na mshika dini. Alikuwa Mwalimu Mkuu wakati ule, kengele ikalia, paredi ikapigwa kama Jeshi usu vile, nikaitwa mbele.

Nilikuwa viboko havina idadi maana walijua kabisa Ile barua lazima wahuni walisaidiana kuisuka na kweli wahuni wenzangu Fulani watoto wa mjini wa darasa la mbele yangu walinisaidia kuiweka sawa ikatulia.

Niliamua liwalo na liwe but kamwe hakuna kuchomesha masela. Vile vibogo vimeniachia alama hadi Leo kwenye nyuma ya mapaja Kwa jinsi nilivyochubuka kama nyoka aliyemwagiwa maji ya moto
 
Kuna wasichana wamepinda,mmoja tulikuwa tunasoma nae kanizidi madarasa 2,alipata skendo ya kubakwa kwenye vichaka vya shule,siku moja akapita karibu yetu tukamtania ,badala ya kuchukia akatufuata na kutuambia ndio lakini nyie hamkuwepo wala msingeweza,daah tukabaki kumshangaa.
 
Ulikurupuka sana, mie nikiwa form 3 nilikula madam mmoja wa biology na mwingine alikuwa wa field. Niliwala sana hadi wanangu walikuwa wanajua maana nilikuwa nawarekodi kimtindo. Na walimu wa kiume walikuwa wanangu sana hata ikitokea soo la kupigwa darasa zima mie walikuwa wananiruka.

Maana nilikuwa nawakopesha sana walimu pesa na nilikuwa siwapangii muda wa kurudisha.
Madam wa biology aliponzwa na simu tu kipindi hiko Sony Xperia Z waterproof akaamua anipe mzigo.
Na madam wa field alitokea tu kunielewa yeye mwenyewe. Code ipo wazi sana ikitokea mwanangu yoyote akisoma hii.
 
Kuna watu automatically ni ma-snitch tu huwa wanazaliwa hivo.
 
Sengerema Sec (Sesesco) mwaka 2003 tulidakwa bwenini muda wa vipindi tena bweni likiwa limefungwa na kufuli, mwalimu wa zamu naona alipewa taarifa kwamba kuna watu huwa wanabaki ndani, akafungua bweni akapiga msako sisi tulivyogundua hilo tukapanda juu ya dali, snitch mmoja ambaye alikuwa kiranja akamsanua ticha kwamba wanajifichaga 'room7' yaani dalini. Kikanuka, tukashuka 'tulikuwa wanne', moja kwa moja kwa Headmaster, kengele Ikalia, stiki zikatembea na suspension juu[emoji16]🥲
 
Bila shaka ni mbeya huku na mkongoraa
 
Hio ni saa saba mchana kipindi kwenye ratiba ya shule kinasoma 'Dini/religious period'. Mimi, demu wangu na mwanafunzi mwenzetu wa kike tume 'camouflage' kwenye jengo Moja la darasa ambalo bado linajengwa.

Hatukupanga tudoji kipindi cha dini ila tumejikuta tu wote ndani pamoja.

Kipindi kikaisha fresh tu bila kusanukiwa, sasa demu wangu bila kujali akaanza yeye kutoka asijue mwalimu wa taaluma alikua nje jirani.

Kuonekana tu nikasikia "wewe unatokea wapi... nyie ndio mnakwepa vipindi vya dini". Shemeji yenu nae nahisi alishikwa kigugumizi. Naona hakujibu chochote akaamrishwa arudi na ticha alipotoka, Yani ndani ya lile jengo.

Tupo kwenye harakati za kuruka na doja aliyebaki nikasikia " wewe kimbiza mwili umeacha jina". Duh! Kusikia hivo ikabidi tuwe wapole. Nakumbuka ilikua saa 7 kuelekea saa nane. Kengele ya dharula ikagongwa.

Mimi, shemeji yenu na huyo Manzi mwingine mbele ya kundi kubwa la wanafunzi wenzetu. Mwalimu aliyetudaka akaanza, " kila siku tunawambia muhudhulie vipindi vya dini mnatoroka sasa Leo wenzenu Hawa watawawakilisha".

Alooh! Kusikia hivo nahisi adrenaline level ikapanda. Namuangalia Manzi yangu Wala hata hawazi katulia kabisa. Yule mwenzie kidogo ndio naona Moja haikai mbili haikai.

Tukaanza kulimwa bakora tatu tatu za maana kisha tukaamrishwa kufanye ibada pale na Mimi ndio mchungaji. Mwalimu akakazia, ibada ifate protocol zote ikiwemo somo, sadaka na matangazo.

Asee tulikuwa comedy Ile siku. Lile jambo lilichukua dakika 15 tukamalizia na bakora za kuagana tatu tatu. Toka hio siku nikaanza kuitwa mchungaji.
 
Mna vituko nimecheka

Ile wengine uandishi unatupa uchovu wa kusoma kumalizia shidaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…