Ulifanya kosa gani Shuleni Hadi kengele ya dharura ikagongwa watu wakaja mstarini kwa ajili yako?

Ulifanya kosa gani Shuleni Hadi kengele ya dharura ikagongwa watu wakaja mstarini kwa ajili yako?

Kuna siku moja tukiwa tunarejea nyumbani baada ya masomo kipindi hicho nipo O-level, ulikuwa msimu wa mahindi bado mwezi kama mmoja kuanza kukomaa. Njia tuliyopita ilikuwaa na mashamba mengi ya mahindi, rafiki zangu watatu walisogelea shamba na kuvunja mihindi kwa ajili ya migagi (ina radha kama miwa kwa mbali), baada ya hapo mimi kama mla doria nikawa nawapa ishara, baada ya dakika kama mbili hivi walitoka jamaa wawili wanakimbia kutoka upande wa ndani wa shamba wanawafuata wadau waliokuwa wanavunja mahindi.

Ili kuepuka kesi mimi na jamaa mmoja ambaye alikuwa ameshika mabegi ya rafiki zetu waliozama ndani wala hatukukimbia tulikaa kimya tu. Jamaa wale wawili walikuwa wanachomoka kama mshale kuwasaka wale wash' kaji zetu.

Baada ya kukimbizana kwa muda mrefu walifanikiwa kuwakaribia na kuwakalili majina yao kwakuwa walikuwa wakikaa nao mtaa mmoja.

Fast forward Jumatatu imefika majira ya mapumziko iligongwa Kengele wote tukaitwa Assembly ground. Nilipoangalia mbele namuona mwalimu wa nidhamu, jamaa fulani mkaksi levo ya mwisho. Huyu alikuwa akifahamika kwa jina la Mboya, mtaalamu wa Geography.

Wale jamaa waliokaririwa majina yao waliitwa mbele, ghafla waliokuja kushtaki wakadai walikuwepo na watu wengine. Mwalimu akawaruhusu jamaa waje kufanya scanning mstari kwa mstari, hio ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwa kama James Bond, alikuwa akienda mbele narudi nyuma akianza kuangalia nyuma naanza kufunga kamba za viatu 😂😂😂

Baada ya kutokuniona mimi na yule jamaa mbeba mabegi ambaye alikimbilia chooni mwamba alirejea mbele na kuanza kuangaza.

Jamaa zetu walibebeshwa mahindi yote ambayo yalikuwa ya.evunjwa kule shambani. Tulikuja kujua kwamba lile lilikuwa shamba la kanisa, na hao jamaa waliokuwa wakikimbiza rafiki zetu ndio waliokuwa walinzi wa shamba.
 
nilikua nauza mzizi wa kuongeza nguvu za kiume maarufu kama MKONGORA. nilikutwa na hiyo mizizi mfuko mzima ule wa kubebea madaftari ulioandikwa SPORT wenye kamba unavaa kama X hivi. kengele ikagongwa nikapata bakora km 20 na ushee, sitasahau! shule nilikuwa naitwa TIPPU TIPPU kwasababu ya biashara ya MKONGORA.
🤣🤣🤣
 
Hapa ni katika level zote 3 za elimu shule ya Msingi, sekondari na Kidato cha 5 na cha 6.

Mimi nakumbuka niliwahi kamatwa na simu kengele ikagongwa nikaipasua kwa mawe hadharani..
Mimi nilikuwa najulikana najua sana kuchora, sasa kuna siku ikakamatwa picha ya kuchora ya mwanamke yupo uchi, na hapo tupo darasa la tano tu, watu kubanwa kuulizwa wote kimya, ila monitress kubanwa anasema atakuwa incharge tu maana ndio anajua kuchora hapa darasani, aise nilitandikwa nikapelekwa chumba cha walimu nikawa nimepigishwa magoti,
Kila mwalimu akiingia anauliza huyu nae vipi aakionyeshwa ile picha tu na yeye ananimalizia hasira zake.
Ikaitwa assembly nikaja kuokolewa na mdosi mmoja demu, akasema sio huyu nilimuona ahmed wakati anachora ndio ikawa pona yangu, yule muarabu ahmed akafukuzwa shule aise
 
Mi bana siku ya kwanza naingia mchaka mchaka darasa la kwanza ila kimtaa,
kuna dogo alinikanyaga mguu aisee nilipiga mpaka kazimika nikakimbia.
Nikaambiwa nisirudi shule
Maza mwalimu karekebisha nikarudi shule
dawati langu nilikua na madem mgeni cheupee mtoto w! Mwalimu na asunta Mtoto wa tajiri mkubwa tu pale.
Bana miaka minne tunacheza mpira dogo Rafael anataka kulipiza.
Wale madem mi walikua washkaji tu.
Kaleta biff tena alikua anamtaka mgeni kwa lazima,
Mgeni analalamika na alikua cheupe(mbulu)
Aisee siku nilikamata hicho ki raphael nilipondaponda yaani kalitoka pale kamelowa.
Asunta hata aweki neno, alikua black beauty with brain.
Rafael kaenda kuripoti kwa babaake.
Babaake si akaja shule.
Kanitwanga ngumi vizuri tu,
Sikumjibu.
Dingi karudi kakuta nimevimba.
"Mwanangu vp"
"nimepigwa"
Na nani?fulani
Mzee akanunua ugomvi "twende"
Zilipigwa ngumi siku hiyo alipigwa mtu mpaka kakaa chini.
huo ndio ubabe mpk leo naujua
Mzee alitisha sana
 
Mimi nilisuka barua Kali sana ya Mapenzi nikiwa darasa la nne kwenda kwa Binti Moja wa mondo B. Ee bwana ee! Kwanini alitimbe nalo ofisini kwa Maasai Moja mwenye masifa sana na mshika dini. Alikuwa Mwalimu Mkuu wakati ule, kengele ikalia, paredi ikapigwa kama Jeshi usu vile, nikaitwa mbele.

Nilikuwa viboko havina idadi maana walijua kabisa Ile barua lazima wahuni walisaidiana kuisuka na kweli wahuni wenzangu Fulani watoto wa mjini wa darasa la mbele yangu walinisaidia kuiweka sawa ikatulia.

Niliamua liwalo na liwe but kamwe hakuna kuchomesha masela. Vile vibogo vimeniachia alama hadi Leo kwenye nyuma ya mapaja Kwa jinsi nilivyochubuka kama nyoka aliyemwagiwa maji ya moto
 
Nilimchomolea rafiki yangu hela kwenye shati kiutani ilikuwa mapumziko mlangoni mwa darasa ili nimrudishie baadaye,kumbe jamaa kaenda kwa ticha.Tukaitwa darasa letu turudi darasani hapo mimi sijagundua tulichoitiwa na pesa ipo mfuko wa shati, Mara namuona ticha ana bakora na Semeni(rafiki yangu)yupo pembeni hapo nikajua nishayakanyaga basi ticha huku ana rundo la stick akasema aliyechukua pesa ya semeni arudishe kabla sijawasachi wote na bakora zisipopatikana,nikasema sizotoi maana zile bakora zitaniishia,ulipita msako huku natetemeka nikazitoa kwenye shati nikazishika mkononi ile ananisachi mfukoni(monitor)mi nimezishika mkononi mikono juu akasema lete begi hapo ndipo nikafanikiwa kuzirudisha mfukoni.Kilichofuata ni kupigwa fimbo 5 kila mmoja.Nilijisikia vibaya sana wenzangu wakipigwa huku wakilalamika kuonewa.Niliendq nae (kwa saa nane) nikamnunulia mihogo.Baada ya siku 2 nikamrudishia hela akashangaa sana nikamwambia alikurupuka kwenda kwa mwalimu,siri tukabaki nayo hadi tulipomaliza shule kama yupo mhanga wa hili tukio samahani sana.Semeni Jarton Mwakyembe uko wapi mkuu?
Kuna wasichana wamepinda,mmoja tulikuwa tunasoma nae kanizidi madarasa 2,alipata skendo ya kubakwa kwenye vichaka vya shule,siku moja akapita karibu yetu tukamtania ,badala ya kuchukia akatufuata na kutuambia ndio lakini nyie hamkuwepo wala msingeweza,daah tukabaki kumshangaa.
 
Balehe mbaya sana, nikiwa 4m1 nilimpenda madam wangu siku moja nikamvizia akiwa peke yake staff nikaingia nikamwambia ukweli, alooo kwanza aliniwasha makofi huku akipiga kelele akisema " wewe mtoto nitakulaani" kesho yake iligongwa kengele ikaitwa bodi ya shule,Afisa elimu, walimu walikusanyika kama 60 pia waliitwa walimu wa primary kama 30 waje wasaidie kunitandika viboko, nilipigwa sana yaani zaidi ya sana
Ulikurupuka sana, mie nikiwa form 3 nilikula madam mmoja wa biology na mwingine alikuwa wa field. Niliwala sana hadi wanangu walikuwa wanajua maana nilikuwa nawarekodi kimtindo. Na walimu wa kiume walikuwa wanangu sana hata ikitokea soo la kupigwa darasa zima mie walikuwa wananiruka.

Maana nilikuwa nawakopesha sana walimu pesa na nilikuwa siwapangii muda wa kurudisha.
Madam wa biology aliponzwa na simu tu kipindi hiko Sony Xperia Z waterproof akaamua anipe mzigo.
Na madam wa field alitokea tu kunielewa yeye mwenyewe. Code ipo wazi sana ikitokea mwanangu yoyote akisoma hii.
 
Form four hyo tulikuwa wanne tunacheza kamari ya karata class kumbe mjinga mmoja kaenda kutochomea kwa headmaster, kuja class tukadakwa tunaenda ofisin headmaster anasema kiingilio cha kuingia ofisi kwake bakora nne na kutoka bakora nne tena, hapo bakora nje ya adhabu. ikapigwa kaengere tukala stick za kutosha na suspension wiki mbili 😂
Kuna watu automatically ni ma-snitch tu huwa wanazaliwa hivo.
 
Sengerema Sec (Sesesco) mwaka 2003 tulidakwa bwenini muda wa vipindi tena bweni likiwa limefungwa na kufuli, mwalimu wa zamu naona alipewa taarifa kwamba kuna watu huwa wanabaki ndani, akafungua bweni akapiga msako sisi tulivyogundua hilo tukapanda juu ya dali, snitch mmoja ambaye alikuwa kiranja akamsanua ticha kwamba wanajifichaga 'room7' yaani dalini. Kikanuka, tukashuka 'tulikuwa wanne', moja kwa moja kwa Headmaster, kengele Ikalia, stiki zikatembea na suspension juu[emoji16]🥲
 
nilikua nauza mzizi wa kuongeza nguvu za kiume maarufu kama MKONGORA. nilikutwa na hiyo mizizi mfuko mzima ule wa kubebea madaftari ulioandikwa SPORT wenye kamba unavaa kama X hivi. kengele ikagongwa nikapata bakora km 20 na ushee, sitasahau! shule nilikuwa naitwa TIPPU TIPPU kwasababu ya biashara ya MKONGORA.
Bila shaka ni mbeya huku na mkongoraa
 
Hio ni saa saba mchana kipindi kwenye ratiba ya shule kinasoma 'Dini/religious period'. Mimi, demu wangu na mwanafunzi mwenzetu wa kike tume 'camouflage' kwenye jengo Moja la darasa ambalo bado linajengwa.

Hatukupanga tudoji kipindi cha dini ila tumejikuta tu wote ndani pamoja.

Kipindi kikaisha fresh tu bila kusanukiwa, sasa demu wangu bila kujali akaanza yeye kutoka asijue mwalimu wa taaluma alikua nje jirani.

Kuonekana tu nikasikia "wewe unatokea wapi... nyie ndio mnakwepa vipindi vya dini". Shemeji yenu nae nahisi alishikwa kigugumizi. Naona hakujibu chochote akaamrishwa arudi na ticha alipotoka, Yani ndani ya lile jengo.

Tupo kwenye harakati za kuruka na doja aliyebaki nikasikia " wewe kimbiza mwili umeacha jina". Duh! Kusikia hivo ikabidi tuwe wapole. Nakumbuka ilikua saa 7 kuelekea saa nane. Kengele ya dharula ikagongwa.

Mimi, shemeji yenu na huyo Manzi mwingine mbele ya kundi kubwa la wanafunzi wenzetu. Mwalimu aliyetudaka akaanza, " kila siku tunawambia muhudhulie vipindi vya dini mnatoroka sasa Leo wenzenu Hawa watawawakilisha".

Alooh! Kusikia hivo nahisi adrenaline level ikapanda. Namuangalia Manzi yangu Wala hata hawazi katulia kabisa. Yule mwenzie kidogo ndio naona Moja haikai mbili haikai.

Tukaanza kulimwa bakora tatu tatu za maana kisha tukaamrishwa kufanye ibada pale na Mimi ndio mchungaji. Mwalimu akakazia, ibada ifate protocol zote ikiwemo somo, sadaka na matangazo.

Asee tulikuwa comedy Ile siku. Lile jambo lilichukua dakika 15 tukamalizia na bakora za kuagana tatu tatu. Toka hio siku nikaanza kuitwa mchungaji.
 
Mna vituko nimecheka

Ile wengine uandishi unatupa uchovu wa kusoma kumalizia shidaaa
 
Back
Top Bottom