Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Niaje niaje,
Wadau tukumbushane enzi hizo na matukio yetu ambayo ukiwaza sasa hivi unajiona mshamba fulani hivi.
~ Nakumbuka nilitoa hela ndefu ili niungwe Facebook, nikiwaza nataman niende Internet Cafe nikamchape yule dada vibao.
~ Shati yangu ya shule bila kutia blue nilihisi sijatokelezea. Zamani bwana memories zake zinafurahisha na kusikitisha.
~ Nilibugia kuberi nikadhani ni chocolate, kichwa kiliuma sana.
~ Nishawahi lamba mafuta ya Kimbo nikidhani blue band.
Wewe unakumbuka jambo gani?