Ulifanya mambo gani zamani ambayo ukikumbuka unajiona mjinga?

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Niaje niaje,

Wadau tukumbushane enzi hizo na matukio yetu ambayo ukiwaza sasa hivi unajiona mshamba fulani hivi.

~ Nakumbuka nilitoa hela ndefu ili niungwe Facebook, nikiwaza nataman niende Internet Cafe nikamchape yule dada vibao.

~ Shati yangu ya shule bila kutia blue nilihisi sijatokelezea. Zamani bwana memories zake zinafurahisha na kusikitisha.

~ Nilibugia kuberi nikadhani ni chocolate, kichwa kiliuma sana.

~ Nishawahi lamba mafuta ya Kimbo nikidhani blue band.

Wewe unakumbuka jambo gani?
 
Nakumbuka enzo hizo kuchat yahoo messanger. Kulikuwa kunw chatrooms za britney spears sijui madonna mimi nikawa nadhani nachat na britney.
Enzi hizo unavaa kiatu kinaitwa square looking back naona chafanana jeneza.
Unakula tshet za dAdA na jeans za sean jon au phat fam
 
Nilikua nanogewa na michezo nikihisi haja napotezea mpaka nibanwe sana ndo nianze kukimbilia chooni. Kabla sijafika tayari vitu vishajiachia vyenyewe

Nilikua nachezea mboko mpaka najiuliza hivi huyu ni mama yangu mzazi au kaniokota?!

Kwa kiasi nilimsumbua na nashkuru kwa mnyoosho wake kwa wakati huo

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Kwa nini ulichelewa nawe? Tusimulie vizuri basi
 
Zamani Coca-cola soda ilikuwa Ina GESI vibaya mno na sukari nyingi kinyama. Yaani enzi hizo ukifanya kosa Haina haja ya kupigwa, unanunuliwa coca tu. Maana walijua ukishamaliza kunywa wakati wa kubeua itakurarua vikali
 
Zamani Coca-cola soda ilikuwa Ina GESI vibaya mno na sukari nyingi kinyama. Yaani enzi hizo ukifanya kosa Haina haja ya kupigwa, unanunuliwa coca tu. Maana walijua ukishamaliza kunywa wakati wa kubeua itakurarua vikali
Mm had Sasa siwez Yani lazima itanipalia๐Ÿ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ