Ulifanya nini ulipodhulumiwa?

Ulifanya nini ulipodhulumiwa?

Mwanamke wa mithali 31

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2024
Posts
1,159
Reaction score
2,577
Niliwahi kudhulumiwa huko nyuma na watu ambao niliwaamini sana, walinirudisha nyuma kwasababu nilikuwa nafanya kazi ngumu na malipo yalikuwa kidogo mno sana, nilijibanaaa sana sana, nikapata kiasi cha pesa kama laki 6 hivi. Kwangu mimi kwa wakati ule ilikuwa nyingi sana ila nilidhulumiwa yote, na watu ambao niliwaamini sana hata leo wapo bado kwenye maisha yangu sijaweza kuwaepuka, ila Mungu atawalipa, kuna namna niliteseka sana sana ila kwa Neema ya Mungu ilipita ila sijasahau

Safari hii tena nimedhulumiwa na huyu mtu ambaye nilimfanyia jambo la upendo ila ameamua kunitendea ubaya, amenidhulumu kilekile kiasi cha pesa 600,000.

Nilimpa kwa upendo atatue shida zake na arejeshe lakini kaniblock kila mahali, hii hali inanitesa sana kuna namna napata maumivu makali mnooo nikiangalia jinsi ninavyopata pesa kwa shida nateseka, hivi ni kweli unamtendea mtu mtu wema anaamua akudhalilishe, anakulipa mabaya.

EE Mungu wa sifa zangu usinyamaze......daah binaadamu sisi uwiiii

Help me, O LORD my God, save me in accordance with your love. Let them know that it is your hand, that you, O LORD, have done it. They may curse, but you will bless,when they attack they will be put to shame, but your servant will rejoice. My accusers will be clothed with disgrace and wrapped in shame as in a cloak.
 
Pole sana.

Ndio ujifunze kuwa katili. Kuna binadamu ni mithili ya wanyama.

Kama unajiamini upo vizuri kuzichapa nenda kampige kata funua mpaka ajipupulie, ila kama hujiamini basi muachie maulana. Maana hakuna fedheha kama kudundwa ukiwa unadai chako.
 
Niliwah kudhurumiwa huko nyuma,na watu ambao niliwaamini sana, walinirudisha nyuma kwasababu nilikua nafanya kazi ngumu na malipo yalikua kidogo mno sana, nilijibanaaa sana sana, nikapata kias cha pesa kama laki 6 hivi kwangu mimi kwa wakati ule ilikua nyingi sana ila nilidhurumiwa yote, na watu ambao niliwaamini sana hata leo wapo bado kwenye maisha yangu sijaweza kuwaepuka, ila Mungu atawalipa, kuna namna niliteseka sana sana ila kwa Neema ya Mungu ilipita ila sijasahau


Safari hii tena nimedhulumiwa na huyu mtu ambaye nilmfanyia jambo la upendo ila ameamua kunitendea ubaya, amenidhulumu kilekile kiasi cha pesa 600,000

Nilimpa kwa upendo atatue shida zake na arejeshe lakini kaniblock kila mahali, hii hali inanitesa sana kuna namna napata maumivu makali mnooo nikiangalia jinsi ninavopata pesa kwa shida nateseka , hivi ni kweli unamtendea mtu Mtu wema anaamua akudhalilishe, anakulipa mabaya

EE Mungu sifa zangu usinyamaze......daah binaadamu sisi uwiiii
Help me, O LORD my God,save me in accordance with your love. Let them know that it is your hand, that you, O LORD, have done it. They may curse, but you will bless,when they attack they will be put to shame, but your servant will rejoice. My accusers will be clothed with disgrace and wrapped in shame as in a cloak.
Maisha hayahitaji hurumahuruma hata kidogo bali umakini na roho ngumu... Kuliko umkopeshe mtu bora umpe kama msaada ili kuepusha maumivu na matatizo pande zote.

Uliemkopesha anapoteza muda kukukwepa huku akiwa na hasira na wewe japo unamdai yeye anaona ulikosea kumkopesha
Kadhalika upande wako ndio kabisa unaumia kwa huruma zako za ajabuajabu.
Waache wafe kuliko uwakopeshe bora uwape kama msaada watakutakia mema

Ni ushauri tu ndugu mimi mwenyewe nateswa na huruma kama wewe 😆
 
Baada ya kukosa usingizi usiku wa manane nilinyoosha mikono juu nikasema.
Eeh Mwenyezi Mungu fulani kanidhulumu, yeye anapata usingizi mimi nakosa usingizi kwakua sina cha kumfanya, Basi nakuachia wewe kwakua ndo hakimu wa haki.

Dua'atu al-muzloom la turad(Dua ya aliedhulimiwa hairudi bila majibu)

He came looking for me and asked for forgiveness.
 
Baada ya kukosa usingizi usiku wa manane nilinyoosha mikono juu nikasema.
Eeh Mwenyezi Mungu fulani kanidhulumu, yeye anapata usingizi mimi nakosa usingizi kwakua sina cha kumfanya, Basi nakuachia wewe kwakua ndo hakimu wa haki.

Dua'atu al-muzloom la turad(Dua ya aliedhulimiwa hairudi bila majibu)

He came looking for me and asked for forgiveness.
MUNGU YUPO HAKIKA
 
Nilipiga magoti magoti kumshukuru Mungu kwa ile dhuluma, yaliyofuatia kwake ni kuyumba kwa project mazima.

kibaya mpaka leo hatambui kama alinidhulumu,
Jamaa yangu tulidhulumiwa wote hana hamu na yule mtu, utasikia "fulani sio mtu yule"
Tulimwamini sana, ila yeye hakuona hilo,
With me karma is real.
 
Baada ya kukosa usingizi usiku wa manane nilinyoosha mikono juu nikasema.
Eeh Mwenyezi Mungu fulani kanidhulumu, yeye anapata usingizi mimi nakosa usingizi kwakua sina cha kumfanya, Basi nakuachia wewe kwakua ndo hakimu wa haki.

Dua'atu al-muzloom la turad(Dua ya aliedhulimiwa hairudi bila majibu)

He came looking for me and asked for forgiveness.
Hebu waombee na wanasiasa waache kutudhulumu 😊
 
mkuu ukarimu kupindukia sometimes unacost sana, unamsaidia mtu mkunjufu tena unayemuamini kabisa then harudishi hata mia zaidi atakublock na kukuepuka
Sasa mwenye kosa ni wewe... Unaweza kukopa bank bila kuweka dhamana ya vitu?
Bank ina hela kuliko wewe lakini hawatoi mkopo bila bond yenye gharama kuliko mkopo wenyewe
 
Back
Top Bottom