Mimi: Hello
Yeye: Hello
Mimi: D... hapa.
Yeye: Nimeijua sauti yako. Shida?
Mimi: Umepita muda mkubwa hatujaonana. Unakumbuka nilikua nikifika hapa uwanjani naongea na wewe mpaka nikifika home?
Yeye: Enhe?
Mimi: Nipo hapa na wewe ndiye pekee nimeona nikupigie tupige stori mbili tatu.
Yeye: Hivi huna haya?
Mimi: (Kimoyomoyo) Enhee.
Yeye: Yaani tangu kipindi kile ndiyo leo umeona leo upige simu? Hivi hata una akili kweli? Mbona watu wengine mnajishushia heshima hivyo? Too bad hata sura yako haifananii matendo yako.
Mimi: Muda huu kwa kilichotokea una haki ya kusema kila kitu. In fact uko sahihi kwa kila unachosema. But just keep me company nivuke huu uwanja.
Yeye: (Huku kabana pua) Eti just keep me company. Company hiyo kwio?
Mimi: Hahaha this is what I missed the most.
Yeye: Achana na mimi...
Mimi: The fact that I've called inamaanisha siwezi.
Yeye: Yaani kila nikikumbuka ulichofanya nashindwa kuamini, wewe kweli?
Mimi: True nimezingua. Ukivumilia next six minutes nakua nimemaliza uwanja.
Yeye: Mmmxxxccccciiiuuu.
Mimi: Hujaacha tu kusonya kwa nguvu hivyo?
Yeye: Mpoleee kumbe loooh.
Mimi: Anyway, so hautaki kunisikiliza?
Yeye: Sema..
Mimi: Nishasema. Nimesema nimekumiss.
Yeye: Asante.
Mimi: Hili siyo jibu nililolizoea.
Yeye: So?
Mimi: So naweza kukupigia baadaye nione kama naweza fanya chochote ikasaidia kupata jibu nililolizoea?
Yeye: Unipigie baadaye ili iweje?
Mimi: Si nimekwambia sababu lakini?
Yeye: Kama unapiga we piga tu ila hayo mengine utajaza mwenyewe.
Mimi: Ok, nakupigia saa nne usiku.
Yeye: Muda huo hapana.
Mimi: Kwanini? Umeolewa tayari?
Yeye: Hata kama ningekua sijaolewa nishakua mkubwa kupigiana simu mida hiyo siyo ishu tena.
Mimi: Mmhh Si mchezo. Haya poa baadaye.
Yeye: Poa.
Baada ya kukata simu. Natext.
'Pale umesema umeshakua ...'
'Nini?'
'Nawaza kama kuna extra kuliko nilichowahi ona'
'Yaani ndiyo mawazo yako hayo.'
'We ungekua mimi ungewaza nini sasa? Chura kama huyo.'
'Hivi bado tu unapenda chura?'
'Naachaje?'
'Duh kazi ipo.'
'Hii kazi ndo nimekuletea wewe'.
Natuma voice note;
🔊
Anajibu.
🔊🔊
Naijibu na mimi.
🔊🔊🔊.
Anajibu kwa text..
'Haiwezi kua.'
Natuma tena voice note:
🔊🔊
Anajibu:
'Nitakushtua'