Habari jf
Katka kupambana na maisha kuna malengo tunajiwekea Shida ni changamoto ya kuyafikia. Mwanzo mwa mwaka 2016 nilijiwekea target kufikisha milion 3.
Kwangu ilikua hela nyingi coz nilikua nasoma na hela ambazo nilikua nashika ni laki laki mwisho laki 5 balance ya akiba laki moja!!... Lakini baadae nilipataga kazi kwaiyo kushika milion 3 ikawa siyo kazi but siyo akiba!! Unakuta hiyo milion tatu ndio ufanye kila kitu akiba au saving ndo laki 3 au 5.
Najaribu kupambana nifike milioni 10 wapi!!
Kila ikifika milioni 3 au 4 napata shida natumia. Sasa nilitaka tubadilishane experience na wanajf wenzangu ambao mmeshavuka huko au mna idea
Nb: Hapa naongelea saving, hela unayoisave baada ya kufanya mambo mengine.
Je, wewe ulifikishaje milioni 10 yako ya mwanzo?
Mkuu Kwa serving ya kupitia mshahara ni ngumu, unless Uwe unapata net pay ya kuanzia 5M kuendelea.
Nakushauri badala ya kuweka Benki ili zijae tafuta namna ya kuzizungusha. Ongeza muda wako WA kufanya kazi toka masaa nane au kumi na mbili upate walau masaa 48 ndani siku ya moja yenye masaa 24, inaweza kuonekana kichekesho fulani lakini ukweli ndo huo.
Namna ya kuongeza masaa ya kufanyakazi ni kuwa na kazi nyingine ndogo ndogo ambazo zitafanywa na watu wengine ambao watakusaidia kuingiza kipato na faida kidogo. Wataalam wa mambo ya fedha Kwa lugha ya Malikia wanaita Levarege,
Chukulia mfano METL kila sekunde moja kuna product yake inanuliwa ambayo pengine inampatia shilingi moja Tu ya faida fanya hesabu upate Kwa Siku anaingiza faida ya shilingi ngapi.
Jambo lingine Acha kuomba muda wa kazi za ziada kazini kwako, badala yake huo muda utumie kufanya shughuli zako. Punguza muda wa kukaa na marafiki baa, punguza magroup ya kuchangiana nk.
NJIA RAHISI NA NYEPESI
Hii njia niliwahi kuitumia wakati nahitaji kukusanya hela Kwa ajili ya kwenda chuo:-
Jiunge na Saccos ambayo inaaminika na ambayo siku ukiamua kujitoa unachukuwa share zako zote. Utafanyaje? Ukishajiunga endelea kuweka share zako jaribu kuweka kile kiwango unachohitaji kufanya serving kila mwezi, hii itakuwezesha usitoe na kitumia hiyo hela hata kama utakuwa na Shida ya kufa, make sheria hazitokuruhusu. Lakini utakuwa na wigo wa kupata mkopo na kutatua matatizo madogo madogo huku akiba yako ikiendelea kusimama. Epuka mkopo mkubwa ambao utavuruga utaratibu wako wa serving ya kila mwezi hasa kipindi utakapokuwa unarejesha deni.
La mwisho na gumu ni kuwa na roho ngumu, Acha kufanya hela yako iwe ya ukoo, hela yako ibaki kuwa ya kwako. Tenga makundi ya lazima ya kuisaidia kama wazazi Kwa pande zote mbili endapo umeoa na uwe na kiwango maalumu.
Mwisho Mimi milioni kumi yangu ya Kwanza nilipata Kwa kulipwa mafao yangu ya PPF baada ya kufanya kazi miaka 7.
Bahati nzuri ni kwamba mwajiri aliuza kazi zilizokuwa chini ya Idara niliyokuwa nafanyia kazi, na zikawa zimechukuliwa na outsourced company. Hivo nilikomba mpunga wangu PPF na nikaendelea na kazi ya mkataba under outsourced company. Nadhani Sisi ndo tumechukuwa hela mwisho kabla ya hizi sheria kandamizi za kuzuia FAO la kujitoa.