Mwaka 2016 baada ya kumaliza chuo,Maisha yalikuwa magumu Sana,nilikuwa siwezi hata kupata vocha na Kula kulikuwa ni kwa manati.nikaanza kufanya kazi za saidia fundi,,KWA KWELI NILIDHARAULIKA SANA PALE MTAANI!!,niki-apply kazi siitwi hata kwenye interview,nikipeleka CV door to door,wanaishia tu kusema CV ni nzuri lakini kazi sipewi!!home hali ni Mbaya,nikimuangalia mama nasikitika sana, mana Kipindi niko shule ilikuwa inafika kipindi anauza ardhi na vitu muhimu ili nisome, lakini ajira hakuna!!Mwaka 2017 nikaweka vyeti pembeni nikaanza kuokota vyuma chakavu(screper)kwenye Madampo na Mahali popote pale nitakapo pata ilimradi tu isiwe ya kuiba,ilikuwa ni fedheha lakini nilikuwa sina namna nyingine,mwezi wa Saba nikawa nimefikisha tani1½ nikauza nikapata laki5,baada ya hapo nikanunua piglets8 wa kienyeji@30000,nikatumia kama Laki2½ hiv,2wakafa maana nilikuwa nawafuga kibabe, wakabaki6 nikawakuza hadi mwezi3,2018,nikaja kuuza kila mmoja lak1.75 nikapata million 1na elf50..nilikaa mwezi mzima nikitafakari ni biashara gani naweza kufanya..baada ya hapo niliamua kufanya biashara za kujumua mpunga mwezi 5,,nikawa naenda Mbalari na Kamsamba-ya ziwa Rukwa.nilikuwa nachukua shambani kwa Bei rahisi nakuja mjini Mbeya nakoboresha nauza. Mwezi wa 9 pesa ikawa imeshakua million 2.8.msimu wa mpunga ukawa umeisha.nikarudi home kutafakari tena nifanye nini..siku moja napitia baadhi ya timu barani ulaya na africa nikaona Kama Kuna fursa flani,.(maana wakati niko kwenye msoto,ilibidi nijifunze kubeti) ,nikasema potelea mbali wacha nirisk elf 30 leo,nikaingia parimatch wakati ule walikuwa hawakati Kodi nikaweka Odd 35.6,KWELI NIKAAMINI MWENYE NACHO HUONGEZEWA,,tiketi ika-WIN nikapata mili1.10 hiv.,wakati nafanya kazi za saidia fundi hakuna tiketi niliyo bet na ika-WIN..na hakuna pesa niliyopata kiurahisi Kama hii..baada ya hapo nikawa nafanya scalping natafuta odd ndogo nastake pesa kubwa nikakuta pesa inakuwa kiutani utani hadi najishangaa..sikumoja nikajiRISK tena nikaweka STAKE ya mill.2 kwa ODDS.3 nikapata milioni 6,sikuamini Kama ni pesa yangu,,NIKAJIULIZA MBONA KIPINDI KILE KWENYE MSOTO MAMBO HAYAKUWA HIVI,?!maana niliitumia takriban karibu miezi7 kupata Tani moja ya vyuma chakavu!!BAADAE ukafika msimu wa kilimo Nikaenda Mbeya vijijini kulima viazi mviringo nikatumia Kama milio1.8,nikavuna nikapa millioni3.4.mpaka Sasa naendelea kujishughulisha na kilimo ufugaji na NA PESA YANGU TAYARI ILISHAVUKA MILION10,naelekea 20mill.