Ulifikishaje Milioni 10 ya kwanza?

Kila mtu amefikia hiyo 10m kwa namna yake.
Ukisema ufanye saving usipokuwa na mikakati madhubuti utazeeka bila kuifikia.

Mimi kazi yangu ya pili yaani cotract nilipaisha hadi 20m kwa wakati mmoja hiyo ni baada ya kutoa kila kitu katika matumizi ya muhimu na ya kawida.

1. Nature ya kazi yako inaweza kukufikisha pale au

2. Kwa kuweka kwenye fixed account na ukawa mwaminifu katika saving.
 
Inahitaji upambane sana, kujinyima vingi
 
Badili id...siwezi kumwamini mtu anajiita mbu...wewe si mnyonyaji damu na mleta maradhi ya moyo tu?
Haya pendekeza jina la ID nzuri uipendayo na uniambie nawezaje kuedit Id yangu ya zamani kuwa mpya.
 
Nilifungua account ya saving nmb na ndio natumia kusevu hadi sasa ,hio haina makato na hauwezi kutoa hela atm wala sim banking unaruhusiwa kuchukua fedha mda wowote ila itakubidi uingie ndani bank physically,ukifungua hio account unakua na atm card kwa ajili ya kuangalia salio tu,nidhamu kali ya matumizi ya fedha inahitajika.
 
Hongera sana,nauliza ulikuwa unatumia njia gan kuwafundisha
 
Una principle nzuri ,napenda kujua ukisema una nunua investment una maanisha nn..
 
Ila kikoba kinasaidia mtu ambaye hawezi kutunza ela yake...maana hupati ela ya ziada na faida ni ndogo sana ukilinganishana riba kama ni lazima kukopa...
 
Mwaka Jana ndo nilishika kwa pamoja kwa mara ya kwanza ila mpaka time hii nimebaki na laki 9 pesa yote imeingia kwenye investment ya maana hope this year ndoto kutengeneza akiba ya 15M+ hapo baada ya matumizi yote.2025 ndo utakua mwaka wa kuvuna zaidi kwasababu biashara nilizowekeza zitarudisha majibu naamini.

Njia iliyotumika nilikua nahifadhi pesa zangu timiza ya Airtel money na nyingine niliweka kwenye kibubu na nyingine Nia sista wangu aliniingilia vikoba somewhere. Mwaka huu nimeingia mwenyewe kikoba.
 
Baada ya kufukuzwa kazini kutokana na mgomo tukalipwa million 8 na hela za nssf ikawa imefikia million 10 ila mpaka leo sijui nilizitumia vp zile hela.
Duh aise...mimi nilipata hela za nssf mil 11 na kitu so nilichofanya sikutaka kukurupuka na biashara mpya nikachukua mil 5 nikaweka utt mfuko wa ukwasi..pesa mil 2 nikafanya mambo yangu na kumaliza deni la kiwanja then mil 4 zilizobaki ndo nazungusha kwenye biashara na faida naiona...pesa za haraka zinapotea kama upepo maaana unaona nying sema ukitulia zinakusaidia.

Faida ya hizo pesa zinazotokana na business nacheza hii michezo ya kina mama kwa mwezi lak 2 ili pesa iwe kwa mzunguko isitumike sehem sio sahihi...
 
Safi sana kiongozi kanyaga twende tumechelewa mnoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…