Uliijuaje JamiiForums?

Uliijuaje JamiiForums?

Nilikua namuona rafiki yangu kipindi hicho ana Blackberry kila mara yupo jf nikajiunga lakini sikuwa na mda nayo sana ad pale nilipokua nikitafuta baadhi ya mambo mtandaoni naletewa kutoka jf. Hapo rasmi nikawa active member na Nokia yangu 5200 enzi hizo hakuna bundle unaweka vocha unaitumia mpaka inaisha. Mpaka sasa nshabadili ID mara 4. ID yangu ya kwanza ilikua ni jina langu halisi mwaka 2010-2011 kama sijakosea.
 
Haki Jf haiboi bana
kuna watu ukisoma post na comments zao unatamani tu kujua ilkuaje mmekutana JF

kwa heshima na taadhima naomba wakuu wafuatao watupe mkasa wao walifikaje fikaje JgF

Kiranga Da Vinci XV Smart911 CHIEF MKWAWA
Mkuu mimi nilikuwapo Jamboforums, ilipopitia mgogoro ndiyo ikaibuka Jamiiforums nikawa grandfathered in.

Niliijua Jamboforums kutokana na mtanange mmoja kati ya Field Marshall ES na Nyani Ngabu

Enzi za "kumkoma nyani giladi".
 
Habari za muda huu waungwana, wanachama na wapenzi wa Jamiiforum,

Ikiwa leo ni zaidi ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwa Jamiiforums, mtandao huu umekuwa kwa kasi sana miongoni mwa Watanzania na wanajamii ya East Africa kwa kuwa Mtandao wa huru na wa haki.

Binafsi naweza sema ni Mtandao wangu pendwa kuliko yote, kwani imekuwa kama kilevi kila nikiwa na bando lazima nichungulie Jamiiforums kuna nini.

Licha ya Mtandao huu kuwa mkubwa hadi kufikia kuwa na watumiaji takribani 632,335 (kwa taarifa za saa 14:20 06/04/2023), bado sio maarufu miongoni mwa Watanzania wengi na hivyo kuwa kama Mtandao fulani wa kisiri ama usiokuwa na wafuatuliaji wengi (unaweza thibitisha hili kwa kuangalia watu wanaokuzunguka na ufahamu wao juu ya Jamiiforum).

Lakini pia miongoni mwetu tunao members waliokuwa bega kwa bega toka miaka ya 2008 na wamesimama na Jamiiforums kwa kipindi chote, huku kila mmoja anahistoria yake ya namna alivyoijua Jamiiforums na hadi kufikia kuwa member kindakindaki.

Uzi huu ni maalum kwaajili ya kuchangia ni kwa namna gani tulikutana na Jamiiforums na hadi sasa tunanufaika vipi, je tunajivunia?

Nianze na mimi Rashmane;

Nakumbuka ilikuwa mwaka 2017 nikiwa na simu yangu ya kibatani, sina bando, nimeboeka nikaingia freebasics bana walau nipate kuijua dunia.

Wakati naperuzi huku na huku nikakutana kwa mara ya kwanza na JamiiForums na zaidi nilivutiwa na nyuzi za Jamii Intelligence na Educational Forums.

Mwaka 2018 nikafungua account hadi sasa tuko pamoja kuisapoti JF paka iwafikie Watanzania wote kwa ujumla, kwani huu ni Mtandao super hapa Tanzania.

Karibuni kwa maoni na mchango wenu.

Uliijuaje JamiiForums?[emoji441]

NB:
Kama kuna member unatamani kufahamu alifikaje JF waweza kumtag

Mshana Jr
Asante Rashmane mimi naomba nitaweka kisa kwa urefu panapo majaliwa[emoji1545][emoji1752][emoji1548]
 
Mkuu mimi nilikuwapo Jamboforums, ilipopitia mgogoro ndiyo ikaibuka Jamiiforums nikawa grandfathered in.

Niliijua Jamboforums kutokana na mtanange mmoja kati ya Field Marshall ES na Nyani Ngabu

Enzi za "kumkoma nyani giladi".
duh salute kwako mkuu

kuna watu humu Jamiiforums wameanza nayo kitambo sana
Hata content zinaakisi uhalisia
 
Ilikua kila nikisearch kitu Chrome lazima jamiiforum ilete majibu, ikiwa kwenye list ya makala zingine zilizojitokea ko kaz Kwangu kuchagua.

Nikawa naichagua Na ilinipa majibu sahihi na yenye ukweli mtupu. Hii ilidumu Kwa miaka kadhaa bila kujua kumbe Kuna hata MASWALA ya kua na account??

Sikumoja mwka Jana nipo stressed sana na jambo Fulani nakasech kitu google kama kawaida kikaitika kupitia JF nkasomaa wee mara nikajaribu kuuchunguza mtandao ndipo nkaona kumbe Kuna App kabisa, kumbe Kuna kua na ID ukawa member, ewaa hapohapo nikaingia na I'd ya MR. KENICE.
 
Me hapo zamani 2014 nilikuwa nafuatilia weekend stories za Lara 1, kwaiyo nilikuwa msomaji tu.. Mpaka 2019 mwisho ndy nikajoin rasmi.

Kama wengine nimefuta apps za social medio karibia zote ila JF tu ndy nipo nayo na naipenda sana.
 
karibu new old member 😅
Ilikua kila nikisearch kitu Chrome lazima jamiiforum ilete majibu, ikiwa kwenye list ya makala zingine zilizojitokea ko kaz Kwangu kuchagua.

Nikawa naichagua Na ilinipa majibu sahihi na yenye ukweli mtupu. Hii ilidumu Kwa miaka kadhaa bila kujua kumbe Kuna hata MASWALA ya kua na account??

Sikumoja mwka Jana nipo stressed sana na jambo Fulani nakasech kitu google kama kawaida kikaitika kupitia JF nkasomaa wee mara nikajaribu kuuchunguza mtandao ndipo nkaona kumbe Kuna App kabisa, kumbe Kuna kua na ID ukawa member, ewaa hapohapo nikaingia na I'd ya MR. KENICE.
 
Nilikuwa nikitafuta kitu moja ya sites ambazo zinatokea jf inakuwepo
Unakuta kile ninachotafuta nikipata najikuta naangalia na vingine ndio ukawa mwanzo wa kuijua hii site 2015 ndio nikawa active kusoma tu mwaka jana naona nimekuwa addict wa kusoma na kulike 😁
 
Back
Top Bottom