Uliijuaje JamiiForums?

Uliijuaje JamiiForums?

Upande wangu nilibahatika kuona stori za MMU zikanivuta na kujoin Jamiiforums.

Nilipata bahati pia ya kupata likes za kutosha kutoka kwa big boss Maxence Melo na akina Invisible, nikawa napambana kucomment ili nipate likes hahahahaaaa....
 
Mwaka 2008 nilifundishwa na luten nyingo (now ni kanal na yupo kozi akiwinda kuwa brigedia)
Aliniambia niangalie list ya matajiri kwa kupitia Google katika orodha ikatokea na jamii forum akafurahi saana kuona habari za kiswahili japo walikuwa wanachangia watu 3 mpaka 10 tu

Mwaka 2010 nikajiunga officially ila sikuwai kuchangia zaidi ya kusoma tu
Kuchangia rasmi nilianza mwaka 2016

Mpaka sasa Nina I'D 34 ila nyingi zao sikumbuki password zake
watu sampuli yako ndio mnafanya tuonekane tupo wengi JF
😅
 
Mwaka 2008 nilifundishwa na luten nyingo (now ni kanal na yupo kozi akiwinda kuwa brigedia)
Aliniambia niangalie list ya matajiri kwa kupitia Google katika orodha ikatokea na jamii forum akafurahi saana kuona habari za kiswahili japo walikuwa wanachangia watu 3 mpaka 10 tu

Mwaka 2010 nikajiunga officially ila sikuwai kuchangia zaidi ya kusoma tu
Kuchangia rasmi nilianza mwaka 2016

Mpaka sasa Nina I'D 34 ila nyingi zao sikumbuki password zake
Ila mkuu umetisha yaani una ID 34 duu
 
Nilikiwa kwemye bar matako bar Arusha mwak 2015 ndipo muhudumu nikamuona ana app ya jf nikashangaa kajuaje mtandao ambao nilwai kuusikia kuwa Ni Moto balaa ndipo na mm kimy kimya nikafuta app ila kuwa rasm Ni 2019

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mwaka 2009 nikiwa form II nilikuwa nikisikiliza radio BBC SWAHILI nikasikia habari kumhusu Maxence Mello na mtandao wa Jamii Forums ndipo nikaifahamu na nilikuja kujiunga rasmi mwaka 2015
 
Binafsi ilikuwa mwaka 2013 wakati nipo kidato cha kwanza, wakati huo simu yangu ya kwanza kuitumia ikiwa ni NOKIA X2, na katika pita pita zangu uko Google kimsingi sikumbuki nilikuwa na search kitu gani.

Ndipo nilipokutana na habari yenye title ' wa mwisho ndo mshindi' then nikaamua kuifungua aisee nilivutiwa sana na huo mchezo kuanzia hapo nikawa ni mara kwa mara naingia JF ila sikuwa na acount kwa muda huo but acount yangu ya kwanza humu niliifungua 2015.

Huu uzi wa mwisho ndo mshindi ulinifanya wakati nimemaliza kidato cha nne ile time tunasubiri matokeo nimpate mrembo wa darasa letu alooh alikuwa hapendi kuchati ila kidume nikaamua kumfundisha uzi huu binafsi ili nimpate na tulikuwa tunachat mpaka tunapitiwa na usingizi hadi alikuja kunibariki tunda.

Wakati huo jukwaa langu pendwa likiwa ni JF Social Forums (Lounge) JF chit chats and jokes pamoja na mapenzi mahusiano na urafiki.

Vipi wewe uliifahamu vipi JF?
 
JF niliifaham wakati nmefika chuo ile kugoogle maswali nikawa nakutana na nyuzi zimefafanua vizuri nachokitafuta.
 
Nilikuwa kwenye giza! Siku moja mzee mmoja kaniambia "unaijua JF" nikamwambia ni nini hiyo? Kuna jamaa anaitwa Kiranga anapinga sana uwepo wa Mungu. Kwa kuwa nilipitia kidogo kuhusu mwamba Karl Marx, nikaona nijiunge na JF, mpaka leo sibanduki JF. Idumu JF.
 
Back
Top Bottom