Ulijipata kimaisha ukiwa na miaka mingapi?

Ulijipata kimaisha ukiwa na miaka mingapi?

P h a r a o h

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
785
Reaction score
1,413
wakuu kama mnavyoona zimebaki siku mbili tu kuumaliza mwaka 2024 na kuanza mwaka mwingine 2025,

watu wengi hua wanajiwekea malengo mbalimbali wakiamini mwaka mpya unavyoanza ni rahisi zaidi kuanza mambo mapya au kubadikisha lifestyle ya zamani na kuanza mpya. inaonekana ni rahisi kuliko kuanzia katitati ya mwaka.

lengo hapa ni kupeana experience,

Kuna watu wana malengo au vitu wanavyopanga kuvifikia baada ya mwaka au miaka kadhaa ijayo kuanzia sasa,

Mfano, kufungua biashara ya ukubwa fulani, kujenga nyumba au kumiliki ndinga ya ndoto yako,

Sasa pia kuna watu hizo stage walishazipitia miaka iliyopita na sasa wapo kwenye level nyingine, wamejipata ( kila mtu ana mtizamo wake kuhusu level ambayo atasema amejipata )

Je ulijipata ukiwa na miaka mingapi ?

uliajiriwa au ulifanya mishe kama biashara, kilimo, ufundi n.k ?

ilikua bahati au uliweka plan na mikakati ya kutosha na je uli wahi kufeli mara ngapi ?

Kabla ya kujipata maisha yalikuaje na je uliamini utafikia hapo ulipo ndani ya muda huo ulioutumia kufika ?

Uliwahi kuwa kwenye addiction zinazo kupotezea hela mfano pombe na starehe nyingine wakati bado hujajipata ?

Lengo ni ku share experience na mindset kwa wote wanaojitafuta na ambao wana mipango na melego fulani wanayotamani kuyafikia, kwakua tumetofautiana level ni wazi kua kuna wengi wameshafikia hapo ambapo mwingie bado anapafikiria namna ya kufika.
 
UMRI KATI YA MWAKA 1 MPAKA MIAKA 18.
Huu ni umri wa kujidanganya sana na kutengeneza malengo ya ukubwani na kwanini kujidanganya?

UMRI KATI YA MIAKA 20- 30 (UMRI WA UHALISIA)
Huu ndio umri wa kuona vitu kwa vitendo kwa namna kijana alivyojichora akiwa na miaka 18 kurudi nyuma. Kwenye umri huu ndio utaona maisha ni mstari mnyoofu ama ni mstari wenye kona nyingi?

Katika umri huu mambo mengi yanakuja kinyume na namna mtu alivyofikiri

UMRI KATI YA MIAKA 40- 55.
Huu ni umri wenye matukio mawili makubwa la kwanza ni kukubali matokeo huku ukilazimisha uendelee kuonekana kijana wa miaka 30 ,hii ni wale ambao walikata tamaa na kuona maisha ndio haya haya hivyo wanaamua kuridhika lakini changamoto nyingine inayowakabiri ni kupingana na umri yaani hawataki kukubali kuwa wao ni watu wazima
Changamoto kubwa kwenye umri huu ni kuwa majukumu yanakuwa mengi sana hivyo utegemezi unakuwa mkubwa hivyo kama hukujipanga vizuri utakuwa unapata pesa ila zinaishia kwa wategemezi wako.

UMRI KUANZIA MIAKA 60 KUENDELEA.
Hapa ni uzee tu na kupumzika ijapo bado kuna wengine wataendelea na kutafuta tu kama matokeo ya kushindwa kutumia ujana wao vyema au kushindwa kuweka mikakati mizuri ujanani.

C&P Ishi humo
 
2024 ni hatua Moja nimesonga ,japo wezi walijaribu kunirudisha nilipotoka ilaa ckutaka kurudi ,nimekomaa nikasimama Kwenye hatua yangu Moja niliyoianza 2024 ..Kwa Sasa c habaa nilipotoka na nilipo n hatua....

Vijana tusiache kupeana madili pale unapona unaweza muunganisha mwenzio akapata ridhikii,,na vijana uaminifu uwe ngao yetu tuache TAMAA ya kuiba Kwa watu mnaoonganishwa kupata kazi

Km n kijana umeamua kupambana ndugu wazime cm Kwa muda na wasiwe sehemu ya utafutajii wako na wasijue mambo Yako ..ila km Kuna misiba na sherehe shiriki pita hv ........n hayo tu Kwa 2024
 
Mi nilijipata nikiwa na miak 21 and now nina 29 so nina nyumba mbili moja iko tabora nyengine Dar kigamboni kule karibu na namiliki gari mbili moja ya biashara nyengine ya kutembelea na biashara zangu ziko kariakoo kilichobaki n kuoa tu ndo sijakamilisha
Njia zipi ulipita tupe experience au kuna namna watangulizi wako walikuwa financially stable ukatengenezewa njia tangu upo mdogo wakakukabidhi ulivyojitambua.

Hebu tupe uzoefu mkuu share nasie tuone wapi tulikwama.
 
Mi nilijipata nikiwa na miak 21 and now nina 29 so nina nyumba mbili moja iko tabora nyengine Dar kigamboni kule karibu na namiliki gari mbili moja ya biashara nyengine ya kutembelea na biashara zangu ziko kariakoo kilichobaki n kuoa tu ndo sijakamilisha
UTadhani ni kweli vile, kumbe kweli.
 
Back
Top Bottom