Ulijipata kimaisha ukiwa na miaka mingapi?

Ulijipata kimaisha ukiwa na miaka mingapi?

wakuu kama mnavyoona zimebaki siku mbili tu kuumaliza mwaka 2024 na kuanza mwaka mwingine 2025,

watu wengi hua wanajiwekea malengo mbalimbali wakiamini mwaka mpya unavyoanza ni rahisi zaidi kuanza mambo mapya au kubadikisha lifestyle ya zamani na kuanza mpya. inaonekana ni rahisi kuliko kuanzia katitati ya mwaka.

lengo hapa ni kupeana experience,

Kuna watu wana malengo au vitu wanavyopanga kuvifikia baada ya mwaka au miaka kadhaa ijayo kuanzia sasa,

Mfano, kufungua biashara ya ukubwa fulani, kujenga nyumba au kumiliki ndinga ya ndoto yako,

Sasa pia kuna watu hizo stage walishazipitia miaka iliyopita na sasa wapo kwenye level nyingine, wamejipata ( kila mtu ana mtizamo wake kuhusu level ambayo atasema amejipata )

Je ulijipata ukiwa na miaka mingapi ?

uliajiriwa au ulifanya mishe kama biashara, kilimo, ufundi n.k ?

ilikua bahati au uliweka plan na mikakati ya kutosha na je uli wahi kufeli mara ngapi ?

Kabla ya kujipata maisha yalikuaje na je uliamini utafikia hapo ulipo ndani ya muda huo ulioutumia kufika ?

Uliwahi kuwa kwenye addiction zinazo kupotezea hela mfano pombe na starehe nyingine wakati bado hujajipata ?

Lengo ni ku share experience na mindset kwa wote wanaojitafuta na ambao wana mipango na melego fulani wanayotamani kuyafikia, kwakua tumetofautiana level ni wazi kua kuna wengi wameshafikia hapo ambapo mwingie bado anapafikiria namna ya kufika.
Nilijipata nikiwa na 22,nikalost nikiwa 32,sahivi nipo 37 bado sijarudi kwenye game,nimebaki na nyumba,pikipiki na mtoto mmoja.Mapambano yanaendelea till end of time
 
Nilijipata nikiwa na 22,nikalost nikiwa 32,sahivi nipo 37 bado sijarudi kwenye game,nimebaki na nyumba,pikipiki na mtoto mmoja.Mapambano yanaendelea till end of time
dakika ya 22' ulikia unaongoza 2 - 0 mara paap dakika ya 32' 2 - 1

dakika ya 37' bado tupo katika kipindi cha kwanza cha mchezo
 
Exactly ni kweli hilo suala kwa sababu utoboaji wa maisha kwa ufupi tunatofautiana ndo maana kuna madaraja, hivyo tunaomba kweli njia moja wapo ambayo ilikuwa best mpaka wewe umefika hapo ulipo
Njia zipi ulipita tupe experience au kuna namna watangulizi wako walikuwa financially stable ukatengenezewa njia tangu upo mdogo wakakukabidhi ulivyojitambua.

Hebu tupe uzoefu mkuu share nasie tuone wapi tulikwama.
 
Back
Top Bottom