Ulijipata kimaisha ukiwa na miaka mingapi?

Ulijipata kimaisha ukiwa na miaka mingapi?

Unaweza ukajipata ukiwa chuo tena kwa pesa ya boom ukiwa timamu na uchumi.
Ni kweli japo inahitaji akili nyingi. Nakumbuka nilimalizaga chuo na mtaji wa milioni 5 na pesa za matumizi kiasi kama laki 5 plus assets kama kiwanja na vitu baadhi vya kuanzia maisha.
Ila dah nilijichanganya padogo tu nikajikuta napiga reverse ya hatari..
 
Ni kweli japo inahitaji akili nyingi. Nakumbuka nilimalizaga chuo na mtaji wa milioni 5 na pesa za matumizi kiasi kama laki 5 plus assets kama kiwanja na vitu baadhi vya kuanzia maisha.
Ila dah nilijichanganya padogo tu nikajikuta napiga reverse ya hatari..
Pole mkuu nafasi bado ipo
 
2024 ni hatua Moja nimesonga ,japo wezi walijaribu kunirudisha nilipotoka ilaa ckutaka kurudi ,nimekomaa nikasimama Kwenye hatua yangu Moja niliyoianza 2024 ..Kwa Sasa c habaa nilipotoka na nilipo n hatua....

Vijana tusiache kupeana madili pale unapona unaweza muunganisha mwenzio akapata ridhikii,,na vijana uaminifu uwe ngao yetu tuache TAMAA ya kuiba Kwa watu mnaoonganishwa kupata kazi

Km n kijana umeamua kupambana ndugu wazime cm Kwa muda na wasiwe sehemu ya utafutajii wako na wasijue mambo Yako ..ila km Kuna misiba na sherehe shiriki pita hv ........n hayo tu Kwa 2024
Wezi sio watu poa kabisa Mkuu, tuzidi ku push hard kiongozi
 
Bado napambana, nilianguaka nikasimama nikaanguka tena nikasimama, sasa hiv nimekaa kweny mstari ila maisha haya.

Unakomaa na kitu halafu kinakukataa, baadaye unapojaribu harakati zngine unashangaa vle mambo yanajiset mpka unataman kuuliza ilikuwaje nikaachwa niteseke vile.

Najiona nikienda kujipata, ingawa nilipoteza muda kufosi ambapo sipo.
 
wakuu kama mnavyoona zimebaki siku mbili tu kuumaliza mwaka 2024 na kuanza mwaka mwingine 2025,

watu wengi hua wanajiwekea malengo mbalimbali wakiamini mwaka mpya unavyoanza ni rahisi zaidi kuanza mambo mapya au kubadikisha lifestyle ya zamani na kuanza mpya. inaonekana ni rahisi kuliko kuanzia katitati ya mwaka.

lengo hapa ni kupeana experience,

Kuna watu wana malengo au vitu wanavyopanga kuvifikia baada ya mwaka au miaka kadhaa ijayo kuanzia sasa,

Mfano, kufungua biashara ya ukubwa fulani, kujenga nyumba au kumiliki ndinga ya ndoto yako,

Sasa pia kuna watu hizo stage walishazipitia miaka iliyopita na sasa wapo kwenye level nyingine, wamejipata ( kila mtu ana mtizamo wake kuhusu level ambayo atasema amejipata )

Je ulijipata ukiwa na miaka mingapi ?

uliajiriwa au ulifanya mishe kama biashara, kilimo, ufundi n.k ?

ilikua bahati au uliweka plan na mikakati ya kutosha na je uli wahi kufeli mara ngapi ?

Kabla ya kujipata maisha yalikuaje na je uliamini utafikia hapo ulipo ndani ya muda huo ulioutumia kufika ?

Uliwahi kuwa kwenye addiction zinazo kupotezea hela mfano pombe na starehe nyingine wakati bado hujajipata ?

Lengo ni ku share experience na mindset kwa wote wanaojitafuta na ambao wana mipango na melego fulani wanayotamani kuyafikia, kwakua tumetofautiana level ni wazi kua kuna wengi wameshafikia hapo ambapo mwingie bado anapafikiria namna ya kufika.
Bado nasoma alama za nyakati naamini ntajipata tu kwa hizi hersal z ote
 
30 years now bado sijakaa kwenye line nnayoitaka
Nimeajiriwa,
Kikubwa niicho nacho ni viwanja kadhaa + saving kwenye UTT,
Sijaoa, sina Mtoto na pia mahusiano nliyonayo hayana afya

Kwa kifupi bado na struggle
 
Unaweza ukajipata ukiwa chuo tena kwa pesa ya boom ukiwa timamu na uchumi.
Duh mkuu, hii mbinu mm ndio nmeishtukia round hii baada ya kuingia 2nd year aisee, najuta kwann sikuwa na moto huu milio nao sasa tangu nikiwa 1st year 😳

Kwa kifupi Boom kwa upande wangu nimeliongezea herufi 1 mbele baada ya kuliita MA ( Meals and Accommodation) naliita MA& Personal development 😂
 
Back
Top Bottom