Ulijipata kimaisha ukiwa na miaka mingapi?

Unaweza ukajipata ukiwa chuo tena kwa pesa ya boom ukiwa timamu na uchumi.
Ni kweli japo inahitaji akili nyingi. Nakumbuka nilimalizaga chuo na mtaji wa milioni 5 na pesa za matumizi kiasi kama laki 5 plus assets kama kiwanja na vitu baadhi vya kuanzia maisha.
Ila dah nilijichanganya padogo tu nikajikuta napiga reverse ya hatari..
 
Pole mkuu nafasi bado ipo
 
Wezi sio watu poa kabisa Mkuu, tuzidi ku push hard kiongozi
 
Bado napambana, nilianguaka nikasimama nikaanguka tena nikasimama, sasa hiv nimekaa kweny mstari ila maisha haya.

Unakomaa na kitu halafu kinakukataa, baadaye unapojaribu harakati zngine unashangaa vle mambo yanajiset mpka unataman kuuliza ilikuwaje nikaachwa niteseke vile.

Najiona nikienda kujipata, ingawa nilipoteza muda kufosi ambapo sipo.
 
Bado nasoma alama za nyakati naamini ntajipata tu kwa hizi hersal z ote
 
30 years now bado sijakaa kwenye line nnayoitaka
Nimeajiriwa,
Kikubwa niicho nacho ni viwanja kadhaa + saving kwenye UTT,
Sijaoa, sina Mtoto na pia mahusiano nliyonayo hayana afya

Kwa kifupi bado na struggle
 
Unaweza ukajipata ukiwa chuo tena kwa pesa ya boom ukiwa timamu na uchumi.
Duh mkuu, hii mbinu mm ndio nmeishtukia round hii baada ya kuingia 2nd year aisee, najuta kwann sikuwa na moto huu milio nao sasa tangu nikiwa 1st year 😳

Kwa kifupi Boom kwa upande wangu nimeliongezea herufi 1 mbele baada ya kuliita MA ( Meals and Accommodation) naliita MA& Personal development 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…