Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 9,397
- 12,415
Wakuu,
Katika maisha kuna mambo ambayo huna budi kuyaamini tu, hata kama umehadithiwa na hukuyashuhudia mwenyewe. Kwa mfano, mtu akikuuliza:
“Ulijuaje kama mwaka wako wa kuzaliwa ni sahihi?”
Ukweli ni kwamba, wengi wetu hatujawahi kushuhudia siku tulipozaliwa; tunachokijua ni kile tulichosimuliwa na wazazi wetu, ndugu, au vitambulisho tulivyopatiwa. Tunaamini bila shaka yoyote, japo hatuna ushahidi wa moja kwa moja.
Ukitafakari kwa undani, utagundua kwamba karibu mambo yote tunayoyajua hapa duniani tunayasikia kwa kusimuliwa au kufundishwa. Hata yale tunayofundishwa darasani, ikiwemo sayansi, ni hadithi na maarifa tunayopokea kupitia vitabu na walimu wetu, halafu tunaamua kuyaamini.
Huwezi kuelewa wala kuendelea na masomo kama vile kemia bila kuwa na imani na kile unachofundishwa. Lazima ukubali na kuamini maelezo ya walimu na vitabu, hata kama hujawahi kushuhudia mwenyewe majaribio au matokeo yake.
Vivyo hivyo, Biblia imeandika mambo mengi ambayo kwa mtazamo wa haraka yanaonekana kama simulizi tu. Lakini nakwambia, kila kilichoandikwa katika Biblia ni kweli na hakika. Hakuna uwongo ndani yake; yote ni ukweli mtupu, hata kama hatujashuhudia wenyewe.