Ulikuwa mpenzi wa gazeti gani miaka ya nyuma?

Alasiri na dar leo
 
Mzee mwenzangu kwangu Mimi Bongo,sani na Tabasamu ndio yalikua majarida yangu.Kwa kweli Ile mipicha ya totoz kwenye cover nimejichukulia sheria mkononi sana coz ndio ilikua balehe imepamba moto.
 
Siku ya Alhamisi ni RAI "nguvu ya hoja" chini ya mhariri John Bwire na Sanifu chini ya Munga Tehnani.
Gazeti la kila siku ni Majira.
Majarida ni SANI chini ya Said Bawji na mchoraji mwandamizi Philip Ndunguru na Tabasamu chini ya Masasi na mchoroji John Kaduma.
 
Wewe haujui magazeti jinsi yalivyo! Ni wazi haukuwa msomaji wa magazeti wala msikilizaji wa habari kwenye redio.
 
Sanifu lilikuwa bonge la gazeti. Ule ukurasa wenye Tolu wa Ajabu ulikuwa mtamu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…