Yoso
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 954
- 1,417
Alikuwepo Mwandishi mmoja anaitwa Munga Tehnan km siyo ni Marehemu ?Gazeti la jitambue
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alikuwepo Mwandishi mmoja anaitwa Munga Tehnan km siyo ni Marehemu ?Gazeti la jitambue
Kumbe shujaaz nao wakongwe eeh?na kuna vile vijarida vya shujaaz magari ya coca cola yalikuwa yakileta soda shule yanakuja navyo vingi
View attachment 3219722
Femina.
Femina - it's a magazine.hilo ni jarida au gazeti?
Habarini wakuu!
Hakika miaka inakwenda. Miaka ya nyuma, magazeti yalikuwa na mvuto sana kuanzia front pages hadi ndani. Yalikuwepo magazeti mengi sana ila Binafsi nilikuwa mpenzi wa magazeti ya Sani na Kiu.
Hao jamaa walikuwa wabunifu sana, kurasa za mbele zilipambwa kwa picha nzuri za mastaa na vichwa vya habari vyenye kuibua hisia sana. Picha za warembo wenye maumbile mazuri na muhtasari wa habari zilizomo ndani yake. Raha ya haya magazeti ilikuwa ni zaidi hata ya kumiliki smartphones siku hizi ambazo ni kama zinaleta depression tu kwa watu. Enzi hizo hakukuwa na mambo ya kuwaza sijui fulani hajaview status yangu, mbona hajanipost, sijui kaniblock na mambo kama hizo
Kulikuwa na simulizi zilizotungwa kwa imahiri, zinazokuachia kiu ya kutaka kufatilia toleo lijalo bila kukosa. Pia kulikuwa na katuni kama vile Lodilofa, Kipepe, Kifimbo Cheza, Madenge, Baba ubaya na nyingine nyingi. Hakika ilikuwa zaidi ya burudani.
Leo nimepita ukurasa fulani nikakutana na picha za katuni za enzi hizo nikapata kurejesha kumbukumbu nyuma sana jinsi burudani hizo zilivyoweza kukonga nyoyo zetu. Hiyo ni kwa ufupi tu.
Wewe unakumbuka nini kuhusu magazeti ya enzi hizo?