Ulikuwa na ndoto za kuwa nani utakapokuwa mkubwa? Umeiishi ndoto yako au maisha yamekupeleka kwingine?

Ulikuwa na ndoto za kuwa nani utakapokuwa mkubwa? Umeiishi ndoto yako au maisha yamekupeleka kwingine?

Nilitamani kuwa mwandishi Wa habari Leo nimekuwa Mchungaji.. Bado namshukuru Mungu maana naandika na kureport habari za Yesu.. ndoto imetimia na kuzidi.
 
From ERB to NBAA.

God is good all the time,all the time God is good.
 
Primary nlikuwa na ndoto za kuwa mwanajeshi, secondary nikataman kuwa daktari, baada ya form 4 nkaenda art na huko nkabadilisha ndoto na kuwa HR na asaiv naendelea na ndoto yangu japo nataman kuwa HR na mhadhiri wa chuo
 
Nilikuwa na ndoto ya kuwa rubani ila saivi Nina ndoto ya kuwa billionaire tu
 
Alhamisi inaendaje wakuu?

Tukiwa watoto kuna hili swali huwa tunaulizwa shuleni au hata nyumbani tu, "Fulani ukiwa mkubwa unataka kuwa nani?" Wengine huwa na majibu ya kazi nzuri nzuri na wengine majibu huwaacha hoi wanaosikiliza majibu yao.

Mimi nilikuwa na ndoto za kuwa Daktari, lakini baada ya hesabu na masomo mengine ya sayansi kunipiga roba ya mbao ya hatari nikaachana na ndoto hiyo, sasa nafanya kitu tofauti kabisa na ndoto niliyokuwa nayo.

Wewe ulikuwa na ndoto ya kuwa nani ukiwa mkubwa? Umeiishi ndoto yako au mambo yalikuwa meusi ukafanya mambo mengine?
Naiishi kwenye chaguo langu la 3 maana vikwazo vya machaguo ya kwanza. Aaaaaah😂🤣
 
Nikiwa, darasa la saba, siku ya mtoto wa, Afrika, sherehe ilifanyika UDSM, Nkrumah, nilivutiwa na nikasema, lqzima nifike chuo, nikiwa, form one, nikasema, lazima niwe engineer, nilipokuwa chuo, nikasema, nataka kuwa engineer lakini ndani ya, jwtz!
Siku, nimeenda kufatilia nafasi, pale jkt karibu na kawe, kwanza mapokezi, wakaniuliza, kabila langu! Nikawauliza kabila LA nini? Wakasema litanisaidia, kupata, kazi, kiurahisi,nikapiga chini, nimejaribu Mara nne nafasi ya jeshi, natoswa!
Nikarudi, chuo, ongeza, elimu, niwe muhandisi, nafurahi nimefanikiwa kuwa muhandisi,
Ila bongo fulsa ni chache,kuna watu wana uwezo, makubwa, lakini hawa patients nafasi
Kna ajira na fursa elewa hilo so, fursa zipo nyingi kuliko ajira
 
Kutoka ndoto za kuwa mwanajeshi mpaka mgambo wa jiji. Sio mbaya kivile
 
Baada ya kusoma comments za watu humu leo nimeamini msemo wa jitihada haizidi kudra..

Maisha ya kila mtu yalishapangwa ata kabla hujaja duniani tunakuja kutimiza tu au kukamilisha kile ambacho tunapaswa kufanya basi.
 
Ndoto yangu imekuwaga kuwa Mwanajeshi since primary, mpaka leo nimemaliza Chuo kikuu haijatimia bado lakini naamini itatimia with God's grace..
 
Back
Top Bottom