Ulikuwa wapi wakati Ufaransa hii inaitoa nishai Italy Euro 2000

Ndio niko darasa la 7 by that time nimekaza kichizi napiga dua zangu za kutosha Italy wachukue ndoo mara sub inafanyika kaingia mtu ambae nilikujamchukia sana.

Super~sub David Trezguet alisababisha nikalala roho inaniuma sana *****.
 
Nilikuwa barnaba Niko likizo baada ya kufunga shule, siku hiyo nimetoka zangu kucheza fainali ya kombe la kuku tumepigwa 6-1 na jamaa Fulani walikuwa wanajiita BLACK MAMBAZ wakachukua jogoo wao halafu wakatufurumusha na mawe maana yalikuwa ni madingi na ligi ilichezewa mtaani kwao.

Kwanza sikula kabisa usiku, ukichanganya maumivu ya kukosa kuku na ule mzuka wa kusubiria game hamu ya kula itoke wapi, akili yangu ilikuwa inawaza kumuona TH14 akitupia tu basi.

Siku hiyo Zidane alikuwa haoni pakupitisha mipira aliwekwa kwenye giza la catenacio kila akigeuka akiangalia mbele anamuona canavaro na nesta sio henry wala djokerf.

Mpaka dakika 91 baada ya mpira kuanza nawaona wataliano wakijiandaa kushangilia ubingwa wameshajifunga na bendera zao viunoni, nikajua tayari ngoma imelala na pia muda huo Italia alikuwa ametolewa na France world cup iliyopita kwenye robo fainali hivyo ilikuwa ni mechi ya kisasi.

Sekunde 28 za mwisho wataliano hawawezi kuzisahau kamwe katika maisha yao baada ya trezguet kuwavurugia sherehe, dakika tatu baada ya extra time wiltord ana wauwa wataliano kwa goli la dhahabu na mpira unaisha ufaransa anaweka record ya kuchukua euro na WC ndani ya miaka miwili.

Nikiwa kama shabiki mkubwa wa ufaransa naomba sana FIFA waturudishie tena goli la dhahabu, hili dunia iendelee kuona maajabu yalikuwa yanafanywa na ufaransa kipindi hicho
 
Hahaha, wengine ndo kwanza tulikua 'vidudu'. Wachezaji tulikua tunawajulia kwenye stickers tu.
Utotoni mchezaji nliempenda sana alikua ni titi camara ( sina uhakika na spelling).
 
Pole kwa kukosa jongwe (kuku )ila rekebisha hapo Wiltord ndie alie sawazisha kisha trezagoal akakhitimisha shughuli.
 

Ninaamini hata wewe hukuwepo Wakatia Ufaransa inachukua EURO mwaka 2000..

Coz Hicho Kikosi Umekikosa ikimaanisha hukukukiona wala hukuwahi kukijua...

1. Youri Djokaeff hakuwa kwenye first XI bali alikuwa ni Supper Sub...

2. Thiery Henry pia alikuwa hajawa World Class! Kwahiyo alikuwa hana Namba bali ni Sub..

3. Sylvan

Wiltord pia Aliingia Kama Subs na Wala hakuwa katima XI ....

Kwahiyo kabla ya Kupost kwanza Fatilia....
 
Buffon,Barzagali,Georgie,marchisio,Montolivo,Lorenzo,hao ni baadhi
Mkuu acha utani, hao uliowataja hakuna hata mmoja aliyecheza Michuano ya Euro 2000. Buffon aliumia kidole akakosa michuano, hao wengineo hawakuwepo kwenye Euro 2000 achilia mbali hata mwaka 2006 wakati Italy ananyanyua ubingwa wa Dunia.
 
Fainali TH14 na Youri Djokaeff walianza kwenye first eleven
 
Deschamps bado alikuwepo kikosini Mkuu, rekebisha hapo!
 
Buffon,Barzagali,Georgie,marchisio,Montolivo,Lorenzo,hao ni baadhi
Christian abbiat gk
Ciro ferrara
Paolo maldin
Demitri albetini
Canavaro
Paolo negro
Angelo Di livio
Antonio Conte
Inzhagi
Del piero
Gianluca pessotto
Toldo
Nesta
Luigi Di biagio
Mark luliano
Ambrossini
Zambrotta
Fiore
Montella
Totti
Delvicchio
Antonioli
Kikosi kamili cha wajukuu wa mussollin mwaka 2000
 
Kila ninapoona Jina la Thiery Henry popote Lazma ni pay attention, Nikikumbuka ile Pace yake, dribbling na attacking style yake, Nakuja kuamin football ya Leo Misses something, wapo wengi wanaojua zaid yake ila stail yake sijawah kuiona kwa yyt na ndio iliyovutia wengi
 
Wanasema Mbappe ana playing style kama ya king TH14 lakini binafsi sioni mfanano wowote.
 
Mpira ulipokuwa mpira hapo!
 
Ufaransa hiyo kwenye nusu fainali au robo fainali hivi walikutana na Ureno ya Luis Figo, dakika za lala salama Ufaransa wanapata penati na ilienda kupigwa na Zidane, basi wakati Zidane anaenda kupiga penati, Figo akavua jezi yake na kutoka nje ya uwanja maana alijua Zidane hawezi kosa na lazma akipata watakuwa washatoka kwenye mashindano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…