Ulikuwa wapi wakati Ufaransa hii inaitoa nishai Italy Euro 2000

Ulikuwa wapi wakati Ufaransa hii inaitoa nishai Italy Euro 2000

Pana bwana mdogo mmoja baada ya kupitia michango ya uzi huu akawa hana budi ila kutoa salaam ya maamkizi ya heshima kwa wadau humu. Sasa cha ajabu mnaipita tu comment yake bila kujali heshma aliyowapa ningependa kutumia nafasi hii kuwaomba waungwana muitikieni huyo bwana mdogo salaam yake kisha tuendelee.
 
Ufaransa hiyo kwenye nusu fainali au robo fainali hivi walikutana na Ureno ya Luis Figo, dakika za lala salama Ufaransa wanapata penati na ilienda kupigwa na Zidane, basi wakati Zidane anaenda kupiga penati, Figo akavua jezi yake na kutoka nje ya uwanja maana alijua Zidane hawezi kosa na lazma akipata watakuwa washatoka kwenye mashindano.
soccer-euro-2000-semi-final-france-v-portugal-G9CA28.jpg
 
Hapo niliona fainali zote nikiwa dar kweli sijaona kikosi kama hiki cha Taifa maana kilikuwa na kila ufundi .........ilikuwa raha sana kama fainali ya Euro 1999 man United Vs Bayern Munich nalo lilikuwa bonge la game
 
Hakuna Mechi Iliniuma kama Fainali ya Euro 2000 nilikuwa siwapend France toka Alivyowafunga Brazil 1998 na akaja fainali akampiga Italy
Italy wanapata Goli Wiltord anaswazisha ngoma inaenda Extra Time
Trezeguet anapiga Bonge la Goli Extra Time.
Dah.. tunatofautiana hakuna fainali ilinikosha km ile, aisee ufaransa hii nilikuwa mnazi hasaaa..
 
Hahaha, wengine ndo kwanza tulikua 'vidudu'. Wachezaji tulikua tunawajulia kwenye stickers tu.
Utotoni mchezaji nliempenda sana alikua ni titi camara ( sina uhakika na spelling).
Sahihi..
 
Ninaamini hata wewe hukuwepo Wakatia Ufaransa inachukua EURO mwaka 2000..

Coz Hicho Kikosi Umekikosa ikimaanisha hukukukiona wala hukuwahi kukijua...

1. Youri Djokaeff hakuwa kwenye first XI bali alikuwa ni Supper Sub...

2. Thiery Henry pia alikuwa hajawa World Class! Kwahiyo alikuwa hana Namba bali ni Sub..

3. Sylvan

Wiltord pia Aliingia Kama Subs na Wala hakuwa katima XI ....

Kwahiyo kabla ya Kupost kwanza Fatilia....

Henry alianza game nyingi tu.. djokaeff alianza fainali
 
Ufaransa hiyo kwenye nusu fainali au robo fainali hivi walikutana na Ureno ya Luis Figo, dakika za lala salama Ufaransa wanapata penati na ilienda kupigwa na Zidane, basi wakati Zidane anaenda kupiga penati, Figo akavua jezi yake na kutoka nje ya uwanja maana alijua Zidane hawezi kosa na lazma akipata watakuwa washatoka kwenye mashindano.

Ilikuwa nusu hiyo mkuu.. figo alinivunja mbavu, ilikuwa ni furaha kubwa sababu mie nilikuwa ufaransa damu..
 
Back
Top Bottom