Ulikuwa wapi wakati Ufaransa hii inaitoa nishai Italy Euro 2000


Mbona Hapo Sijamuona Yule Jamaa Ambaye Half ni Mtaliano and Half ni Mfaransa King Christian Viery???
 
Mbona Hapo Sijamuona Yule Jamaa Ambaye Half ni Mtaliano and Half ni Mfaransa King Christian Viery???
Diego fuser Dino baggio na geuseppe pancora na mtu mkubwa Vieri ambae alivunja mwiko wa makocha kutochukua mshambuliaji anae cheza nje ya Italy haikuwa sheria ila makocha wengi walikuwa waumini wa washambuliaji wanaocheza nyumbani aliumia so katika kundi la watu 26 alikuwepo kisha majeraha yakamtoa .Mtu mwingine alie toka ni gigi buffon yeye alikuwa miongoni mwa 22 ila mchezo wa kirafiki na Norway ukamtoa na nafasi kuzibwa na nyanda wa AC Milan abbiat.
 
Pia tukumbuke Italy imejionyesha siku nyingi kuwa na walinda mlango wazuri toka kwa Dino Zoff chuma hiki miaka ya 80 na alichukua mwali pale Mexico kisha wakaja wadogo zake kama Walter zenga miaka ya 90 baadae ndio wakaibuka kina Angelo peruzzi na Gianluca pagriuca walikuwa wapinzani kweli kabla ya kumuachia mikoba Toldo ambae akaja kuikabidhi kwa gigi.
 
Nusu hiyo makosa yanafanywa na beki abel xavier alikuwa anatia dawa nywele zake na ndevu pia dakika ya 117 likawa tuta nani anaenda kupiga si mwingine ila ni YAZID basi luis figo akaona hakuna haja ya kuendelea kubaki uwanjani mpira umekwisha tena huo na ikawa kama alivyotabiri.
 
Nlikua form 2 those days,Sebule nzima kuanzia dingi mpaka madogo walikua washabiki wa Italy...mi peke yangu shabiki wa Ufaransa..hadi dk ya 90 nimejikunyata km mtoto yatima...wiltod akatutoa kimasomaso
 
Kuna mtu umemsahau, Bernard Lama...golikipa wa akiba.

Achana na hii kikosi
 

Mkuu hapa umesahau Kidogo! Katika Mechi Hii Kipa Hakuwa Chrisrian Abbiati!!! Bali Alikuwa ni Francesco Toldo ambaye walimuumiza mpaka akawa anacheza Game hii akiwa anatoka Damu za Pua huku akiwakatili France Michomo Mikali Waliyokua Wakimpigia...

List Ya Italy ilikua Kama ifuatavyo:-

Francesco Toldo (GK)

Paolo Maldini (C)

Demetrio Albertini

Fabio Cannavaro

Gianluca Pessotto

Alessandro Nesta

Luigi Di Biagio

Mark Iuliano

Stefano Fiore

Francesco Totti (Man of The Match)
 
Ni kweli mkuu, Dino Zoff alitamba wakati Italy ikibeba ndoo ya Dunia pale Espana (Spain) mwaka 1982 chino ya Mshambuliaji matata wa kipindi hiko Paolo Rossi.
Pia kuna beki aliyeitwa Claudio Gentile ambaye alisifika kwa man marking dhidi ya washambuliaji hatari waliokutana na Italy.

Kuna mlinda mlango anaitwa Sirigu alikuja vizuri kumchallenge Buffon ila siku hizi amepotea sana!
 
Abel Xavier alikipiga hadi Liverpool ya akina Titi Camara, Henchoz, Sammy Hyppia.

Yap ilikuwa ni nusu fainali halafu extra time. Asante kwa kunikumbusha!
 
Hakusema mechi ya fainali, anasema kuelekea kwenye michuano hiyo, Buffon aliumia nafasi ikajazwa na Abbiati.
 
Shukran kwa masahihisho 82 ilikuwa Spain na sio Mexico ambayo ilikuwa world cup iliyofuatia yaah paulo rossi alikuwa matata sana.
 
Mkuu ile penati ilikuwa na utata,namkumbuka beki kisiki xzavier,baadaye alikuja kucheza liverpool lkn hakufanikiwa sana hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…