Ulikuwa wapi wakati Ufaransa hii inaitoa nishai Italy Euro 2000

Lazarazu, hunishindi mimi unazi kwa ufaransa. Siku ile David anaunganisha mpira wa kross ya Pires iliyotoka kulia nilipiga kelele nikavua shati mbio mbaya kutoka nje kutamba.

Mimi hata nikifa leo, ndugu na marafiki zangu watanikumbuka zaidi kwa ushabiki wangu uliotukuka kwa timu ya ma black, warabu na wazungu Ufaransa.
 
Ni Christian karembeu sio Patrick pia pana mtu aliitwa johan micoud akina Vincent candela pia walihusika katika squad hii
 
Ni Christian karembeu sio Patrick pia pana mtu aliitwa johan micoud akina Vincent candela pia walihusika katika squad hii
 
Umenchekesha sana kwamba kichogo alikutia matatani
 



Kikosi mahiri sana.
 
Aloo kumbe ni wengi mimi mwenyewe ule wingi wa mablack ulichangia sana kunifanya niwe shabiki wa ufaransa na walikuwa wanapiga kazi haswaa akina Viera na marcelle hawa watu walikuwa ni nadra kumaliza game bila kadi.

Nakumbuka WC ya 2014 kuna commentator alisema 'an african team represents Europe' akimaanisha ufaransa.

Happy to meet my fellow les bleus supporter tukutane russia mwakani kufanya maajabu si unajua tena tukiwa hatupewi nafasi huwa tuna watoa wale wanaopewa nafasi halafu si ndio tunachukua.
 

Ndio ukweli huo.
 
Comrade Lizarazu wewe umeshakuwa ndugu yangu humu jf, mimi mtu yoyote anayeshabikia France humuona ni ndugu yangu.

Baada ya hapo nyuma chama letu kuchuja kidogo sasa hivi lipo on fire. Bara lote la Ulaya chama lenye uimala kama letu ni Germany tu. Hugo Lloris, Sidibe, Digne, Varane, Umtiti, Cante, Pogba, Martial, Mbape, Dembele, Griezmann na Coman hawa ni vijana wabichi na wote wako vilabu vikubwa ulaya. Ukiwaongeza wakongwe akina Matuid, Lucazette, Sissoko, Benzem sioni wa kusimama hapo.

Namchukia sana kocha kuwa anamuacha Bezema na Ben Arfa alafu anamchukua Giroud. Ben Arfa ni kama Halzad, basi tu. Tulikosa kombe la Ulaya kwa sababu ya chuki za kijinga za Dischamps.
 
Rapa Gentamycin, Hivi kile kikosi chetu World Cup 2006 hasimu wetu Blazir angeponea wapi? 1.Bartez, 2.Sagnol, 3.Abidal, 4.Gallas, 5.Thuram, 6.Viera, 7.Marouda, 8.Makelele, 9.Trezeguet, 10.Zizou, 11.Henry. Beanch yuko Ribery farasi, Wiltod, Sirvestre, Coupet na Govou. Hapo Blazir ilikuwa lazima are 16 bora kwenda robo final.

Gaucho wao na Ronaldo walikumbana na kiama cha miamba ya kiafrika yenye nguvu Gallas, Thuram, Viera na Makelele.

Siku ile nilifurahi nilipiga kelele mtaani kama mwehu huku mtaa ukiwa kimya kama wamefiwa eti kisa Blazir kufa. Na hiyo ilikuwa ni mfululizo wa waniga wa kifaransa kumchinja na kumsukumiza nje Blazir world cup, mwanzo ilikuwa 1986 kule Mexico alafu 1998 Ufaransa tena 2006 Ujeruman na kabla ya hapo 2001 Blazir alikuwa amesha uwawa kule Japan robo final ya kombe la mabara wauwaji wakiwa akina Pires na Diessel.

Nawapenda sana Less Blues na huwa nawachukia sana Blazir kwakuwa washabiki wao hawaipendi kabisa Ufaransa yaani wao hupenda Ufaransa tuchapwe na timu yoyote ile tunayokutana nayo.
 
Goli la dhahabu lilifungwa na Wiltold? Au la kusawazisha?
 
Nahisi yupo Crystal Palace
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…