Ulimwengu: Chaumma walipata kura ngapi kuwawezesha kupata wabunge viti maalum?

Ulimwengu: Chaumma walipata kura ngapi kuwawezesha kupata wabunge viti maalum?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Jen. Ulimwengu: Fr. Kitima, Wewe unasema kwamba ulipata takwimu za uchaguzi uliopita.

Fr. Kitima: Zilitangazwa siku kabla ya kuapishwa mheshimiwa rais na waheshimiwa wabunge tulitangaziwa. Mimi nilitegemea nilipata tu kwenye vyombo vya habari. Unajua mimi kwanza siruhusiwi kuobserve sisi taasisi za dini haturuhusiwi na sheria iliotungwa na nyie Watanzania kwamba mashirika ya dini yasiende kwenye vituo vya kura kuangalia nani anapiga kura.

Kwa hiyo hata kama walienda 9 kila kituo 10 au ni 8% nchi nzima walienda hiyo hatukuenda kwa kweli. Hatujui. Ila sisi tulipata tu kwenye vyombo vya habari. Aliyeshinda ni huyu. Chama hiki kimepata hivi, chama hiki hivi. Wabunge walioshinda ni hawa. Kwa hiyo tunafuata hivyo na sisi tunapopewa taarifa zisipopingwa tunaona ni halali.

Ulimwengu: Chauma walipata viti vingapi vya ubunge?

Fr. Kitima: Naomba nisaidiwe hapo

Mshiriki: Kwa sababu Viti vya ubunge wa Viti maalum Viti maalum Viti viwili.

Ulimwengu: Kutokana na viti vingapi vya wabunge kwa ujumla?

Mshiriki: Hapo sasa tume ya taifa tume huru ya taifa ya uchaguzi ingetusaidia lakini walikuwa na mbunge mmoja wa jimbo.

Ulimwengu: Hii ni kweli kwamba viti maalum kutokana na wingi wa wabunge waliomo bungeni sio?

Mshiriki: Idadi ya kura ile wastani ya kura za ubunge.

Ulimwengu: Sasa Chauma walikua na kura ngapi?

Washiriki: Hatufahamu kwa kweli. Hatufahamu.

Ulimwengu: Ndio. Sasa unawezaje kusema kwamba una uhakika Chauma walipata wabunge wawili wa viti maalum kama hujui kura walizopata za kura za wabunge.

Mshiriki: Tumeona matokeo yamewekwa kule umoja wa mabunge duniani wameweka matokeo pale. Wanaelezea matokeo ya uchaguzi mkuu wa Tanzania ulivyoyaenda generally.
 
Back
Top Bottom