Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwanahabari mkongwe, Jenerali Ulimwengu, ameitaka Serikali kuipa nafasi zaidi TBC kufanya kazi kama Shirika la Utangazaji la Taifa badala ya kuonekana kama chombo cha Serikali. Ulimwengu amesema hayo leo, Septemba 28, 2026, katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa kwa Wote, yaliyoandaliwa na Mtandao wa Wadau wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI).
"Najiuliza, hivi TBC ni Shirika la Utangazaji la Taifa au Shirika la Utangazaji la Serikali? Kwa muda mrefu shirika hilo limekuwa si mnyama si ndege, linajinasibisha kuwa la Taifa lakini nikiliangalia naliona ni la Serikali. Kumbuka linaendeshwa kwa kodi za Wananchi lakini kama kitu hakiipendezi Serikali hukioni kwenye TBC.
"Mfano nadhani kilichotokea Oktoba 29, 2025 chochote ambacho kilitokea hakikuipendeza Serikali hakikuweza kupelekwa hewani, mwisho wa siku Shirika linakuwa la CCM. Nadhani CCM iiachie TBC ifanye kazi kama Shirika la Taifa."
Fuatilia hapa >>> Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa kwa Wote, 28/09/2026