Ok bhasi ngoja nikuongezee kitu ambacho unachanganya....
Neno christ limetokna na neno la Kigiriki
χριστός (chrīstós) linalomaanisha Mpakwa mafuta (The anointed one to do some activities) hapa sijui umeelewa..
au kwa lugha ya Kihebrania
מָשִׁיחַ (Mašíaḥ, messiah),
kwahiyo Christ/kristo/kristu ni sawa na kusema Masihi kwa kihebrania
Unaweza ukasoma
Yohana 1:41-42 kupata refference zaidi ya kibiblia ukitaka..
View attachment 2795296
Sasa turudi tuangalia kina nani waliwahi kuwa masihi ama kristo...
Masihi hakuwahi kuwa mtu bali ni cheo cha watu...
Zaburi 105:14-15
"Hakumwacha mtu awaonee,
Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao. Akisema, Msiwaguse masihi wangu, Wala msiwadhuru nabii zangu.."
Ntakutajia Masihi wachache u kama wanne hivi au watano!
Sauli ,Daudi, Samweli, Isaya Na wengi walikuwa masihi wa bwana ( yaani sauli alikuwa kristo) soma zaburi 2:2, zaburi 45:7, Isaya 61:1
1 Samweli 24:6-7
[6]Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.
[7]Basi Daudi akawazuia watu wake kwa maneno hayo, asiwaache kumwondokea Sauli. Kisha Sauli akatoka pangoni, akaenda zake.