Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wadau asanteni kwa shule nzuri hii, ninapata huduma ya azam TV kwa maana ya dish na kin'gamuzi, sasa nataka kupata na channel za soka hasa EPL je naweza kuzipata bila kupoteza za local, msaada tafadhali.
Usipokuwa makini na mwangalifu na ugonjwa wa ASAS unaweza kuwa kama bendera mtu akikuambia tu huku kuna chnl tayari utaanza kugeuza ungo wako bila sababu ya lazima na pengine chnl unayoitafuta haipo katika eneo unaloishi. Tujifunze kutafuta kwanza uhalisia wa habari kabla hatujaanza kugeuza nyungo zetu.
Aidha napenda pia kusema kwa mara nyingine tenakuwa rcva yoyote ya mpeg4 ni mpeg2 na rcva yoyote ya DVBS-2 ni DVBS-1 na kinyume chake si sahihi
Kwa urahisi ni hivi: Mpeg4= wake na mpeg2=wanawake. Ukiwa na mlinganyo huo ni sahihi kusema wake (wanawake walioolewa) wote wa watu ni wanawake ila si kweli kwamba wanawake wote ni wake za watu. Kwa mtazamo huu ndugu josephjul40 bado kuna shughuli kubwa ya kuendelea kueleza mambo ya msingi kabla watu hawajaweza kutega nyungo. Kutegeza ungo inaweza kuwa rahisi sana (kwani watu wengi hufanya kwa mazoea) Layman anaweza kujua kuwa ALU (Artemether Lumefantrie) inatibu malaria lakini hawezi kujua ni kwa namna gani inatibu. Ndivyo ilivyo na kwa watu wanaoweza kutega nyungo kwa mwelekeo fulani. Kama kuna yeyote ambaye haamini ninachosema awe wa kwanza kujibu swali hili : NI KWA NINI UNGO WA PACKAGE YA AZAM UNAELEKEZWA MAGHARIBI WAKATI SATELAITI YAKE IPO MASHARIKI? (NI MUHIMU UNITAJIE SATELAITI HII).Fatilia kuona majibu yatakayoletwa hapa.
Mbona kimya humu.....
Ndugu nashukuru sana kwa elimu mnayotoa, mimi niko Musoma na natumia dish na king'amuzi cha azam. Uwezo wa kulipa kila mwezi haupo maana Azam hamna channel za bure usipolipa tu hata zile wanaita za bure wanafungia! Naomba kueleweshwa kama naweza tumia king'amuzi hiki nje ya mtandao wa azam na nikapata channel za bure
Ndugu nashukuru sana kwa elimu mnayotoa, mimi niko Musoma na natumia dish na king'amuzi cha azam. Uwezo wa kulipa kila mwezi haupo maana Azam hamna channel za bure usipolipa tu hata zile wanaita za bure wanafungia! Naomba kueleweshwa kama naweza tumia king'amuzi hiki nje ya mtandao wa azam na nikapata channel za bure
Daa! hii kitu huwa naivutia subira. Ubaya haina punguzo la Pasaka, Krismas, Sababa, Nanenane wala Siku ya walalahoi. Ngoja niendelee kusubiri.
Kwa dish size gani Dar mkuu?