Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

Mzee nisaidie ni. App gani nzuri inayoweza kusapoti channel Za sport Za afirica
 
Model gani iko vizuri zaidi kwa fta, naona kama decoder za continental ziko model tofauti tofauti.
...
Model CDM YH8216, hii ni combo na kwa matumizi ya continental.
Inapokea fta - free to air na ftv - free to view.
Decoder bora za fta, wasiliana na Mwl.RCT na Wamavoko.
...
 
Habari wadau?
Ninataka nichukue hii decoder ya SKYSAT S2020. Vipi kuhusu ufanisi wake, local chaneli unaweza kupata?. Binafsi ni mpenzi wa ligi za ulaya vipi chaneli za sports zipo?

FTA.PNG
 
Nipe majina yake na makadirio ya bei zake ninunue

Sent using Jamii Forums mobile app
- Kuna Qsat model Q15, Q23, Q26 nk. Hizi bei zake zinaanzia 150,000/- kupanda juu kulingana na model. Hizi ni FTA (HD) lkn Uzuri wake ni kwamba ina unscramble channels zote zilizofungwa kwa PowerVU na BISS key. Hawa hawana decoder feki sokoni.
- Kuna Mediacom 940+, hii nayo ni FTA (HD) na ni nzuri pia, ingawa haina uwezo wa kufungua channels zilizofungwa kwa kwa BISS na PowerVU. Bei zake zinaanzia 95,000/- .
- Kuna Strong SRT 49 series (HD). Hizi ndio baba lao, na ni wakongwe sokoni kuliko hao hapo juu. Bei zao zmeshiba, na zinaanzia 250,000/- ingawa zipo feki nyingi sana. Hizi hufungua channels za FTA na zile zilizofungwa kwa BISS na PowerVu.
- Kuna Azsky G6 (HD), hii nayo inafungua FTA na zilizofungwa kwa BISS. Ni chache sana sokoni, ila bei inaanzia 200,000/-
- Kuna Astrovox (HD), nazo zipo sokoni ingawa sio pupular. Bei zake zinaanzia 80,000/-
- Kuna Starsat 2000 (HD) extreme, bei yake inaanzia 230,000/-.
- OnSat receiver inafungua FTA na canal 22w kwa account. Inauzwa kuanzia 190,000/-.
- Freesat v7 (HD) nayo inafungua FTA. Bei zake zinaanzia 100,000/-.
- OpenBox (HD) hii na yenyewe ina PowerVu,bisskeys, RF na be yake inaanzia 90,000/-.
- Digisat 9800 yenye rf, bisskey nk na bei yake inaanzia 85,000/-.

Nadhani kwa kuanzia unaweza kucheki hizo. Bei zinatofautiana kati ya duka na duka na namna unavyojipeleka.
 
Back
Top Bottom