Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,497
- 4,775
Wizi wa kimtandao umekuwa ni jambo la kawaida sana katika jamii yetu hii inatokana na ukuaji wa teknolojia na uelewa mdogo wa watu wengi katika mayumizi ya vifaa vya kidijitali vya mawasiliano, hii ni mbinu mpya ya kuwaibiwa watu kwa njia ya mtandao huku mwizi huyo akiwa amejificha nyuma ya simu kwa sababu anajua anachokifanya na anajua ni namna gani hawezi kugundulika kwa haraka.
Wizi wa kimtandao unafanyika na wengi wanaibiwa kwa sababu ya uelewa mdogo wa matumizi ya vifaa vya kidigitali ama vifaa vya mawasiliano, kwa kiasi kikubwa jamii yetu , watu wengi wanajua kutumia vifaa vya kidigitali kama njia ya mawasiliano ya kawaida tu, lakini uelewa wa namna gani ya kulinda vifaa vyao, namna gani ya kuvitumia kwa njii iliyokuwa bora na makini ni mdogo sana, hali hii hupelekea wezi wengi ambao ni matapeli kwa njii ya simu kuweza kuwaingiza watu wengi katika mtego na kuwaibia pesa.
Watu wamekuwa wakitapeliwa na kuibiwa pesa zao kwa njii ya kufanya miamala ya simu kwa mikono yao na kutuma pesa inayoingia katika katika mikono ya wajanja wengi wa mjini wanaokula kwa jasho la wengine, wakiiba kwa akili na mipango mikubwa.
JE WEZI WA KIMTANDAO WAMEJIPANGA ?
Wizi wa kimtandao hufanyika kwa watu kujipanga na kusuka utapeli wao kwa kiwango cha hali ya juu, kwa mfano :
Kuna matapeli ambao wao hutumia mbinu ya kuuza simu kwa watu wasiowaju na baadae kutoa taatifa ya kuibiwa simu kwa mamlaka husika, na kisha alieuziwa simu kujikuta akikamtwa kama mwizi, ndio maana inashauriwa kutokununua simu simu mkononi, ukinunua simu hakikisha una nunua dukani , dai risiti.
Matapeli hao ujipanga kwa njia ifuatayo.
Tapeli mmoja hupewa simu kwa lengo la kwenda kuuza mtaani kwa mtu asiemjua, baada ya simu kupata soko, muuza simu, anarudi kwa wenzake na hapo wanagawana mapata, muuza simu anakua kamaliza mchezo wake, na kwa asilimia mia moja, anakuwa na uhakika kuwa aliemuuzia simu hawezi mjua.
Baadae ya hapo, matapeli hao huingia katika mchezo wa pili wa kwwnda kutoa taarifa polisi ya kuibiwa kwa simu, hapo tapeli muuza simu ankuwa ametokomea kusikojulikana.
Polisi watakapoitafuta simu, mwisho watafanikiwa kumdaka mwenye simu na mwenye simu kukutana na kizaa zaa cha wizi na asijue kamuuzia nani.
Kama kawaida ya maisha yetu ya kibongo, mtu ataona kuliko akaishie jela kwa wizi, ni bora wakamalizane kifamilia, hapo sasa tapeli na kundi lake wanajikuta wakitengeneza pesa kwa kutaka upande wa alieuziwa simu kutoa kiasi fulani ili kesi ifutwe, na mwisho simu inarudi na hela zinaibiwa.
Kuna haja sasa ya kuanza kuwafuatilia na wanaotoa taarifa ya kuibadili wa kwa simu, isije kuwa watu wanawafanyia mchezo wa kitapeli watu wengine.
WEZI WA MTANDAO NI KINA NANI NA HUSHIRIKIANA NA NANI ?
Hawa ni watu ambao wao siku yao huisha kwa kutegemea kuwaibia watu kwa njia ya kuwaandikia ujumbe mfupi au kuwapigia simu, wezi hawa wapo wasomi na wenye elimu yao ya juu na wapo wengine wa darasa la saba lakini wenye mikakati ya kitapeli iliyopangiliwa vizuri na kwa umakini wa hali ya juu, japokuwa wapo matapeli chipukizi ambao wao hujaribu kufanya utapeli lakini huanguka dakika za mwanzo kabisa, hawa mipango yao huwa ni midogo mno.
Wezi hawa hufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na watu wawili muhimu sana katika kazi yao, mtu wa kwanza ni Mtu anaefanya kazi ya kusajili laini ya simu (asie muaminifu) huyu msajili wa laini ya simu kazi yake ni moja tu, kuuza taarifa za mteja mwingine na kumpatia tapeli kwa makubaliano kuwa atalipwa kiasi Fulani cha pesa na mara nyingi hadi shilingi 50,000 na zaidi hapo kitambulisho cha mtu Fulani hutumika kufanya usajili kwa ajili ya tapeli huyo, ndio maana unashauriwa sana kuangalia mara kwa mara idadi ya namba zilizosajiliwa kwa taarifa zako.
Baada ya usajili kukamilika kazi ya kwanza ya mwizi inakuwa imesha na hapo anaingia kutengeneza mshirika wa pili muhimu kwake, huyu anakuwa ni mtoa huduma za kipesa ama wakala (wenye maduka na vibanda vya kutolea pesa) kazi yake huyu ni mmoja tu, yeye atakuwa anafanya miamala ya kuhamisha pesa kutoka katika laini iliyosajiliwa na inayotumiwa na tapeli, na zoezi hili hufanyika kwa haraka Zaidi baada tu ya mtu kuwa ameingizwa katika mitego ya utapeli, na baada ya zoezi hili kukamilika, hapo laini iliyofanya utapeli inaweza kutupwa , kuvunjiliwa mbali ama kutolewa hewani kwa sababu lengo tapeli linakuwa limekamilika.
Huyu mtoa huduma ya kifedha yeye anakuwa ni mchezeshaji wa mwisho kabisa na hayupo moja kwa moja katika usukwaji wa mipango ya utapeli, yeye anasubiria tu pesa ziingie katika akaunti ya tapeli na kuifanyia muamala
JINSI MATAPELI WANAVYOTENGENEZA TIMU YAO.
Matapeli wa kimtandao hufanya kazi kwa mikakati mikubwa ambayo husukwa kwa ufundi na mahesabu ya hali ya juu.
Baada ya tapeli kuwa amepata usajili wa laini ya simu na kumuongeza mtoa huduma za kifedha katika timu yao, wanachofanya sasa ni kusuka mpango mwingine wa kuandaa timu yao, ambap kila mmoja anawajibika kulingana na aina ya utapeli wanaofanya.
Kwa mfano, kama wanata kumtapeli mzazi mwenye mtoto anaesoma mbali, basi timu yao inaweza kuwa na watu wawili au watatu muhimu sana, wa kwanza anaweza kuwa mwalimu mlezi (wa bandia) na mwalimu mkuu wa shule pamoja na daktari feki, hawa kila mmoja anakuwa anatumia mawasiliano yake binafsi ila wote wanakuwa wanafanya mchezo mmoja wa kumuingiza mtu mjini kwa kujifanya labda mtoto ni mgonjwa na yuko hospitali na kiasi Fulani cha pesa kinahitajika
Ili sasa kuzidi kumzubaisha mtu, tapeli wa kwanza anaweza kupiga simu au kuandika ujumbe kwa mzazi na kumpa taarifa ya mtoto wake na hapo anaweza kumpa mawasiliano ya mwalimu mkuu, na mzazi anapopiga simu kwa mwalimu mkuu mwalimu atamueleza kila kitu kuhusu mtoto wake na hapo anaweza kumpa mzazi namba za daktari na daktari akawa na jukumu la mwisho la kuumaliza mchezo.
Wakati haya yanafanyika, matapeli wote hawa wanakuwa sehemu moja na wanajua kila kinachoendelea.
Njia nyingine ni kuwadanganya watu kwa kuwapa dili la pesa ama kuwaandikia kuwa wameshinda kiasi Fulani cha fedha, njii hupendwa sana na matapeli kwa sababu wanaamini kuwa watu wengi wanatamaa na wanapowapo dili la fedha basi mtu ataona bora apiganie dili hilo na asiliache lipite bure, mwisho mtu anajikuta gizani.
NINI KIFANYIKE ?
Nina maoni machache hapa, hatua muhimu zaidi ya kuchukuliwa, kwanza kila namba inayohusika na utapeli ifuatiliwe ni nani alieifanyia usajili wake, huyo ataweza kutaja watu anaowauzia taarifa.
Pili makampuni yote ya simu, pindi yakigundulika mtandao wake umetumiwa na matapeli na wakawa hawana taarfia ya nani muhusika katika utapeli huo, basi kampuni hiyo ya simu ikutane na adhabu kali kwa sababu pia inawezekana mambo mengi ya usalama wa watu na hata taifa ukawa hatarini kwa sababu ya udhaifu uliopo katika makampuni ya simu.
NINI UNAPASWA KUFANYA
Kama mtumiaji wa simu, hakikisha namba zako za NIDA hazijatumika kufanya usajili nje ya laini unayotumia, hii itakulinda wewe dhidi ya taarifa zako kutumika vibaya, pia wakati unapofanya usajili wa namba yako ya simu, usikubali kirahisi mtoa huduma akwambie kuwa usajili umekataa hivyo anataka kurudia kukufanyia usajili kwa mara yapili, tatu, usikubali kutuma pesa kwa mtu yeyite usiemjua na mwisho, usiwe na tamaa ya hela za mtandaoni kwa watu usiowafahamu.
Kielelezo
Katika sauti ambazo utakuwa unazisikia hapa, nimefanyia uhariri wa kubadili sauti ili kuficha sauti za wahusika
Sauti hii ya kwanza, ni tapeli aliekuwa anatoa maelekezo kwenda kwa katapeli wa pili, lengo lao likiwa ni kutengeneza uaminifu wa bandia kwa mtu wanaetaka kumtapeli
Kielelezo hiki cha pili ni tapeli wa pili (Anaejulikana kwa jina la kitapeli kama Dr Nasra Abeid) aliekuwa anachezeshwa na tapeli mwenzake wa kwanza, lakini katika sauti hii, ni mwisho baada ya utapeli wao kuwa umeshtukiwa.
Katika sauti inayofuata, jamaa tapeli amejaribu kuelezea namna gani wanavyofanya ili kuweza kuwaingiza watu katika mtego na namna pia wanavyoweza kushinda kesi pindi wanapopelekwa mahakamani.
KUMBUKA
Ili kuwagundua matapeli wa Kimtandao, unahitaji kucheza na akili zao, kumbuka kuwa makini zaidi.

Upvote
6