Ulimwengu wa Roho, Maswali kadhaa ya kutaka kujua ukweli usio na shaka yoyote.

Ulimwengu wa Roho, Maswali kadhaa ya kutaka kujua ukweli usio na shaka yoyote.

Brojust

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
349
Reaction score
1,024
Great thinkers Habari zenu.

Ulimwengu wa roho ni nini kwa kiswahili cha kawaida kabisa, Maswali yangu matatu tu ikiwapendeza naomba mnijibu ?

NB; Rejea za vitabu vya dini zitumike panapo stahili, Ila akili yako huru ndio itatukomboa wengi tunaotaka kujifunza juu ya haya maswali.

1. Ulimwengu wa roho upoje, una fananaje ?

2. Nani ndio kiongozi mkuu wa ulimwengu wa roho.

3. Kama kweli ulimwengu wa kiroho upo je roho inaweza kwenda hadi sayari ya Pluto na ikaja kutoa majibu kwa binadamu kwamba kule sayari ya Pluto kuna nini kunaendelea ?

Ahsante;

NB; Hatutaki ujuaji humu, tunataka great thinkers tu, Tupo kwenye mapambano ya kuirudisha jamiiforum ya Great thinkers tu.
 
Nafikiri ni ngumu kutambua uwepo au kutokuwepo kwa ulimwengu wa roho bila kutumia nguvu ya ulimwengu wa roho.

wengi wetu uamini uwepo wa ulimwengu wa roho kutokana na aadhi ya matukio ambayo hutokea mara chache sana ama kupitia katika ndoto au hisia ambayo hujitokeza katika ulimwengu wa kawaida lakini kwa kumbukumbu za ndoto ni kama picha yake halisi.

mfano unaweza kuelezwa jambo katika ndoto au kupitia nyuma ya hisia halisi na baadaye likatokea kama halisi nk.

Na mara nyingi mtu ukifuata misingi ya ulimwengu wa roho kuendesha maisha mambo mengi yanatokea kama ulivyotaka kama umefuata formula za ulimwengu wa roho.

Ni eneo pana sana ambalo haltakiwi mtu ambaye ni greater thinker kuwa na upande. Ukiamini kama hakuna ulimwengu wa roho kamwe husibeze au kupinga wanaoamini ulimwengu wa roho au kinyume chake.

Kati ya wachungaji bora katika katika kufundisha ulimwengu wa roho ni Sanbela Kyando. kuna viodeo zake nyingi ufundisha kwa mifano kabisa ya uhalisia na biblia. Nkipata moja ya video zake nitakuwekea
 
Great thinkers Habari zenu.

Ulimwengu wa roho ni nini kwa kiswahili cha kawaida kabisa, Maswali yangu matatu tu ikiwapendeza naomba mnijibu ?

NB; Rejea za vitabu vya dini zitumike panapo stahili, Ila akili yako huru ndio itatukomboa wengi tunaotaka kujifunza juu ya haya maswali.

1. Ulimwengu wa roho upoje, una fananaje ?

2. Nani ndio kiongozi mkuu wa ulimwengu wa roho.

3. Kama kweli ulimwengu wa kiroho upo je roho inaweza kwenda hadi sayari ya Pluto na ikaja kutoa majibu kwa binadamu kwamba kule sayari ya Pluto kuna nini kunaendelea ?

Ahsante;

NB; Hatutaki ujuaji humu, tunataka great thinkers tu, Tupo kwenye mapambano ya kuirudisha jamiiforum ya Great thinkers tu.
Kwanza kabisa kuna Ulimwengu mbili wa Roho na wa Mwili
Ulimwengu wa roho ni Ulimwengu usionekana ..
Ulimwengu wa mwili ni ulimwengu unaoonekana.
Ulimwengu wa Roho kwa namna nyingine ni Ulimwengu wa GIZA na Ulimwengu wa mwili kwa namna nyingine ni Ulimwengu wa NURU

Tuuzungumzie huu wa Roho sasa kwenye ulimwengu wa roho kuna tawala mbili Mungu Muumba na Shetani hivyo basi unaweza kuwa kwenye ulimwengu wa roho kwa nguvu ya Mungu au kwa nguvu ya shetani kwasababu wote ni watawala kwenye ulimwengu wa roho hakuna namna nyingine
Kuna watu watabisha ulimwengu wa roho sio ulimwengu wa giza.. sikiliza ukitaka kuomba Mungu lazima ufunge macho ili kulipata giza wale wa ndoto pia huwezi ota ukiwa macho lazima ufunge macho ili ulipate giza sana kuna wale wanaosema maombi ya usiku ndio yenye matokeo zaidi kuliko ya mchana kingine pia Mungu alivyoiumba dunia aliiumbia gizani.. hata upande wa pili nao ni hivyohivyo wanafanyia mambo yao gizani zaidi ili yafanikiwe.. kwanamna nyingine tena ulimwengu wa roho ni Ulimwengu wa Siri wanajua kanuni hii wanafanikiwa kirahisi wasiojua wanatumia muda mwingi kufanikisha ya mambo yao
 
Swali lako la3 ukiwa kwenye ulimwengu wa roho unafika kokote unapotaka kufika saa hiyohiyo maana ulimwengu wa roho hauna muda kama ulimwengu wa mwili ila utakapoenda na kurudi hamna atakae kuamini maana utakao waeleza wako ulimwengu wa mwili na sheria za ulimwengu wa roho na wa Mwili ni tofauti..
 
Samahani mkuu naoma kama unajambo kubwa sana ili utuelezee
 
Back
Top Bottom