Ulimwengu wa roho ni timilifu

Pumba. Asante kwa kunipotezea muda na kujaza seva ya JF...
 
Leo Mshana nakupinga 100%. Kama kila kitu kimeshapangwa basi kuwa na dini hakuna maana kwa vile dini zinatuambia tutende mema. Hapangekuwa na haja ya ibada wala kufunga iwe Ramadhani au Kwaresima. Dhambi ni tendo analolifanya mtu kwa kudhamiria-yaani kwa UAMUZI WAKE. Unaposema kila kitu kimepangwa una maana hata dhambi mtu anazofanya ambazo anaamua kuzifanya yeye mwenyewe kwa utashi wake ni kitu kilichokuwa kimepangwa? Nonsense. Sema Mungu ametupangia kila mmoja maisha mema (na kumpa kila mtu kipawa fulani cha kumfanikisha maishani), lakini shetani (kupitia binadamu wenzetu) anazuia mafanikio Mungu aliyotupangia. Kwa hivyo, mipango Mungu aliyotupangia kweli ipo (na ni mizuri) lakini sio kwamba eti kama ni uovu basi ni Mungu amemuumba mtu ili awe nao. HAPANA. Mungu amemuumba KILA MTU afanikiwe ila ni shetani tu anayeharibu.
 
Hivi ulimwengu Wa roho ndo ulimwengu gani jamani? Tujuzani jamini sisi wengine hatuamini uwepo Wa mungu
 

Kwa mtazamo wangu, ulimwengu wa Roho upo. Ni mazingira (Misingi ya uhalisia ya mazingira yetu) kabla hujaja kwenye mwili tulikuwepo katika ulimwengu wa Roho, na hata vitu vingi kabla havijatokea kwa kuweza kuonekana vinaanzia ulimwengu wa Roho.

Package nzima ipo kuanzia ulipozaliwa, utapita wapi (kuanzia kuzaliwa mpaka utakapokufa/ siku ya mwisho duniani) kwani asili ya kuumbwa kwa mtu kunabaraka ndani yake. Mungu alituleta ili tuitawale Dunia

Kinachotokea baada ya anguko (baada ya kufarakana na Mungu), shetani ndio akatawala Dunia na kumbuka dhumuni la shetani ni kutufarakanisha na Mungu.

Shetani anaweza kuingia katika mfumo wa Mwanadamu na kubadilisha destiny yake, na ndio maana tunaanguka katika dhambi, shetani anaweza kuweka tamaa kwenye moyo wa mtu... ambapo kwa hiyo tamaa ukaaungukia katika mauti.

Waefeso 6:10-12 yasema, “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
 
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Yeremia 1 : 5
 
kwahiyo maisha tayari yapo framed, sisi tunafuata tu kama train kwenye railway!, kwahyo mfano jambazi yeye alipangiwa atazaliwa, ataishi itafika muda ataiba ataua halaf mwisho wa siku motoni, na wengine reli yao imenyooka hadi peponi!?
Dah..... Wahubiri huwa Wanajichanganya sana...... Ukifikiria kwa utulivu utaona dini ni zaka na sadaka tu[emoji87] [emoji87]
 
Ujamuelewa vizuri na Mimi nilipoanza kusoma nikabaki nashangaa nimefuatilia reply zake zote anamaanisha kuwa kabla ujazaliwa Mungu anakuwa amekupangia njia yako utayopitia hadi utakapo kufa na njia hii ni njema maana mwishowe tutauona ufalme wa Mungu.

Tatizo linakuja pale tunapoacha kuufuta mchoro hule ( njia) mana njia hii ina up and down ila ni kwa mapenzi ya Mungu ili mwishoni tufikie destination ya kuuona ufalme wa Mungu think about Yusufu alifungwa hadi gerezani ila ilikuwa kwa mpango wa Mungu think about Samson hizi njia zilikuwa katika mchoro ili wamtukuze Mungu na kumbuka ukifuta mchoro wako lazima ufikie mwisho mwema mana Mungu anatuwazia mema.

Sasa tatizo ni pale ambapo tunaishi nje ya mchoro looh hapo inaitwa kukengeuza unaweza pitia magumu ukamwacha Mungu kumbe ilikuwa ndio pathway yako kuuona ufalme wa Mungu basi tukapanic tukaanza kutafuta nguvu za ibilisi zitupatie maisha mazuri totally wrong.

Cha msingi tusiache kuomba pia na shukuran regardless tunapitia mazingira gani Mungu anatuwazia mema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…