Natamani kuelezea kitu Lakini nashindwa namna ya kuelezea. ila kiukweli kila unachofanya I we kibaya kwa namna ya ufahamu wako, ama iwe unaona ni Chema kwa ufahamu wako, vyote hivyo vilishapangwa tayari na hakuna namna unaweza kukwepa..
Mfano ktk biblia imeandikwa kwamba Yesu alijua kwamba Nani atamsaliti na alimwambia wazi wazi kwamba atamsaliti lakini kwa kuwa tayari ilishapangwa kwamba Hilo jambo litafanyika ktk maisha ya huyo mtu ndio maana wahusika ambao ni Yuda na Petro walishindwa kuzuia isitokee mpaka pale walipo timiza kumsaliti yesu ndio wakakumbuka kwamba tayari yesu alishatabiri kwamba Hilo jambo litatokea. Pia hata yesu mwenyewe alijaribu kuomba kikombe chake cha mateso kimwepuke, ila kwa kuwa anajua kanuni ya maisha akakubali mapenzi ya mwenyezi yatimizwe, maana yake ni kwamba hakuna namna yoyote ya kubadili script uliyopangiwa kuicheza
Anayejiona ni mwana wa Mungu na kuwaona wengine ni wadhambi hiyo ni kutokana tu na namna ya ufahamu wake, na inatakiwa iwe hivyo kwa sababu ndio script yake aliyopangiwa kuicheza na aliye mkuu. Na ndio mana hata ukijiona ni mtu mwema mara nyingi huwa unajikuta pia ukiangukia kwenye mambo mabaya kwa namna ya tafsiri yako ya maisha, ila kiuhalisia yote unayofanya ni marejeleo au matimizo ya unayotakiwa kufanya.