Ulinganisho wa Ofisi za Kaunti ya Machakos (Ksh350 milioni) dhidi ya Ikulu mpya ya Tanzania ya (Ksh175 milioni)

Ulinganisho wa Ofisi za Kaunti ya Machakos (Ksh350 milioni) dhidi ya Ikulu mpya ya Tanzania ya (Ksh175 milioni)

Hivi kwa nini walirudia kujenga Dodoma kama Magogoni??
 
Mnamo mwaka 2020 Gavana wa Machakos Dkt. Alfred Mutua alizindua makao makuu mapya ya kaunti hiyo. Jengo hilo jipya, ambalo linafananishwa na Ikulu ya Marekani - lilifunguliwa rasmi Jumatano, Mei 6, 2020 baada ya ujenzi wake kukamilika kwa gharama ya kiasi cha fedha Ksh. 350 milioni ambazo ni zaidi ya Bilioni 6 za Tanzania.


Mnamo tarehe 20 Mei, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliongoza uzinduzi rasmi wa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma ambapo Rais na watumishi wengine watahamia katika Ikulu hiyo. Ujenzi wa Ikulu hiyo umegharimu zaidi kiasi cha fedha Ksh. 175 milioni ambazo ni zaidi ya Bilioni 3 za Tanzania.

Ikulu ya Serikali iliyoko Dar es Salaam ilijengwa na wakoloni, hata hivyo, Ikulu ya Chamwino inajivunia ujuzi na nguvu kazi kutoka kwa wenyeji kwa kupitia Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania (JKT). Ujenzi huo kutekelezwa na JKT kunaelezwa kusababisha kupungua kwa gharama za ujenzi huo.
Sijaona ubaya wa hili jengo.
Ni zuri na usikute imara kuliko la Kenya.
Ila Kenya wapigaji unajengaje jengo la kawaida kama hilo kwa pesa nyingi hivyo??
 
Utofauti upo ni hivi

Makao ya gavana ni Tsh 300 milion the rest zilienda owa wapigaji means gigantic corrupt

Wakati ikulu ilijengewa kwa pesa halali hakuna kupiga apo .


Au nimekosea

Ni kweli kabisa kaka, wapigaji unaweza kuta wana 50%+ ya hiyo amount waliotaja hapo. Sasa wanajaribu kuilinganisha na ikulu ya Chamwino ili wawaghiribu akili walalahoi wa kenya. Wajione wao wako juu. Teh teh teh.

Ona nyingine hii walivyopigwa.


 
Back
Top Bottom