N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 7,427
- 10,905
Tanki la kuhifadhia Maji la Plastiki dhidi ya tanki la chuma
Unapotafuta tanki la kuhifadhia maji ya mvua au hata ya bomba kwa ajili ya matumizi ya baadae huko sokoni utapata matanki ya kila sampuli ambayo yametengenezwa kutokana na malighafi tofauti. Sasa kwa leo tuangalie haya mawili.
Kama umekuwa ukifanyia utafiti matanki ya chuma cha pua basi utakuwa umeshayaona yale ya kuunganisha kwa boriti ambayo hayashiki kutu (stainless) na haya ya plastiki (poly tanks) ambayo ni mengi utakuwa umeyaona kila sampuli hapa Tanzania yapo kila kona.
Binafsi kwenye ka compaund kangu natamani niweke haya ya chuma...sasa nikasema wacha nilete hii analysis niliyoinasa huko kwa wenzetu.
TUANGALIE SIFA LINGANIFU ZA MATANKI HAYA
Yale ya chuma: Sifa zake

- Matanki ya chuma cha pua yana maisha marefu ya kutoa huduma ya kuhifadhi maji (ingawa yana gharama kubwa unapoyanunua ikilinganishwa na tanki la plastiki ambalo bei yake ni chee).
- Matanki ya maji ya chuma hayawezi kushika moto - labda hii inaweza kuwa faida kwa maeneo ambayo yana moto wa msituni hasa wale ndugu zangu mnaoweka matanki haya kwenye bustani huko maporini kv kwenye bustani za vitunguu nk.
- Kwa kuzingatia kwamba matanki ya chuma ni mazito...ni vigumu kwa wezi kuiba kirahisi ukilinganisha na yale ya plastiki ambayo huibwa mara kwa mara.
- Matanki ya chuma ni vigumu kutoboka kwa muda mfupi na hayaathiriwi pakubwa na joto...tofauti ya yale ya plastiki ambayo hukauka hasa kwenye maeneo ya kitropiki kama Dar es salaam ambako jua huwaka sana.
- Matanki ya Chuma ni rahisi kuyatengeneza yanapopata hitilafu. Ni suala la kumuita mtu wa fabrications au nut and bolt guy anakuja anafix tu mara moja. Unlike tanki la Plastiki likitoboka inabidi uachane nalo...kwa sababu hata likiungwa kwa moto ubora wake hupotea.
- Matanki ya chuma hupunguza uwezekano wa maji kuwa contaminated au kuchafuliwa na fangasi na algae ambao wana athari kwa mtumiaji wa maji
- HIVYO BASI kwa mtazamo wangu nadhani kama una uwezo ni vema kutumia tanki la chuma...japo kwa hapa kwetu Tanzania hayapatikani kiurahisi.
-