Hii ni tofauti kidogo na walinzi wengi wa wakuu wa nchi ambao huvaa miwani maalum myeusi yenye uwezo wa kuvuta taswira ya watu kutoka kwenye hadhara, kupiga picha na wakati mwingine kubaini vitu vya kielectroniki vinavyoweza kuwa tishio.
Lakini kwa walinzi hawa wa Kim Jong-un wao macho yao halisi yanatumika zaidi. Pamoja na uwezo huo, wana uwezo wa kuzima tishio ‘lolote’ kutoka kwa watu wa pembeni dhidi kiongozi huyo kwa kutumia mikono na miili yao, hata kama watu hao wana silaha!
Kati ya walinzi hao wanaokimbia wakitengeneza mzungunguko kwenye gari, lazima awepo kiongozi mkuu wa kikosi hicho kutoka katika ofisi yao kuu kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa, akiongoza na kuratibu kwa kushiriki moja kwa moja. Hivyo, naye ni komando wa makomando mwenye mafunzo ya ziada anayefanya kazi kama maafisa wengine.