UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 51
- 38
Ukisikiliza simulizi za watoto wanaoishi katika mazingira magumu Shinyanga unaweza kujiuliza Serikali iko wapi na inafanya nini kulinda ustawi wao kisheria, kanuni na miongozo mingi mizuri iliyopo kwa ajili yao.
Utafiti uliofanywa na NIPASHE kwa miezi mitatu umebaini sio ongezeko tu la watoto wanaoishi bila uangalizi wa wazazi au walezi, bali wengi wakijiingiza au kushawishiwa kuingia kwenye vitendo vya uhalifu na wengine kudhalilishwa.
Katika utafiti huo, viongozi wa Serikali za Mitaa wamethibitisha pasi na shaka kuongezeka wa idadi ya watoto hao mitaani wakisema wengi wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kama bangi na vitendo vya ngono na ulawiti.
Kanuni za Usalama wa Mtoto za mwaka 2014 (marekebisho 2019) zinabainisha kuwa mtoto anatakiwa kuishi kwenye familia yake na kulindwa dhidi ya aina yoyote ya udhalilishaji wa kingono, awe anafahamu kinachotendeka au la. na ni kinyume kumshawishi mtoto afanye matendo yaliyo kinyume na maadili
Katika Manispaa ya Shinyanga, kanuni hizo zimepewa kisogo, ambapo kumekuwapo na idadi kubwa ya watoto wanaoishi mazingira magumu na kushinda mitaani hovyo kwa ajili ya kujitafutia ridhiki ikiwamo chakula na wengine kuishi kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji kingono.
Mtoto Shabani Ngussa (jina si lake halisi) mwenye miaka 11 mkazi wa Busulwa, anasema yeye anaishi na Bibi yake, na amekomea darasa la pili na kukimbilia mitaani, mara baada ya kuona wanaishi maisha magumu, huku siku nyingine wakilala njaa.
Anasimulia kuwa, maisha ya mitaani siyo mazuri sababu hukumbana na maswaibu mengi, ikiwamo kufundishwa kulawitiana na kuvuta bangi.
“huku mitaani siyo pazuri, lakini angalau tunapata chakula kwa kuomba omba au kula mabaki ya chakula kwenye mahoteli na Stendi za mabasi ambayo abiria hubakiza, kuliko kwa Bibi unalala njaa,”anasema Ngussa.
Mtoto mwingine Abubakari Jonas (jina siyo lake) mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa Ibinzamata, anasema wanapokuwa wamelala kwenye madaraja au majumba mabovu, hukutwa na vijana wakubwa, na kuanza kuwavutishwa bangi na vilevi, na wakilewa ndipo huanza kulawitiwa, na watoto wa kike kubakwa.
“Ukiamka asubuhi na madawa kupungua mwili, ndipo unaanza kusikia maumivu makali huku nyuma, ikifika usiku wanakuja tena na inakuwa kama mazoea, mwisho wa siku na sisi tuna anza kuiga tabia hiyo na kuingilia wenyewe kwa wenyewe, na haya ndiyo maisha yetu brother, ”anasimulia Jonas.
Faustina Kivambe, ni moja wa mashuhuda ambaye anasimulia kuwa alishashuhudia mmoja wa watoto hao akiwa wamefanyiwa ukatili wa kulawitiwa.
Anasema siku moja akiwa kwenye Biashara zake, alimuona moto wa kiume mwenye umri wa miaka mitano, akiwa anatembea na wenzake kama anasikia maumivu makali, ndipo akamuita na kumuuliza, akamwambia jana usiku ameingiliwa kwa nyuma na hana msaada wa kupatiwa matibabu sababu yeye anaishi mitaani tu.
“Roho ili niuma sana kama mzazi, kwa mtoto mdogo kama huyo kufanyiwa kitendo cha kinyama, niliamua kumsaidia, lakini tunaiomba serikali ione namna ya kuwasaidia hawa watoto wanateseka sana na kufanyiwa vitendo vya kikatili,”amesema Faustina.
Kwangu Shidelya ni Bibi ambaye anaishi na Mjukuu wake, anasema aliachiwa na mtoto wake, lakini yeye hana uwezo wa kumtunza, na ndiyo maana humuacha aende mitaani kujitafutia ridhiki.
Anasema, ni kweli watoto kuishi mitaani wanakuwa katika mazingira hatarishi, ikiwamo kufanyiwa vitendo vya ukatili, lakini kutokana na hali duni ya maisha, wanashindwa kuwazuia kwenda huko mitaani.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Busulwa Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga Pastory Kishiwa, anasema katika mtaa huo wapo watoto ambao wanaishi mazingira magumu, na wengi hudhurura hovyo mitaani wajitafutia chakula na mahitaji yao, kutokana na kukosa malezi bora na uangalizi kwa wazazi wao.
Anasema, watoto hao wanapokuwa wakiishi mitaani wengine hujikuta wakiingia kwenye makundi mabaya ya uvutaji bangi, kubakwa kwa watoto wa kike, na wakiume kulawitiwa.
“Visa vya watoto kubakwa na kulawitiwa tumekuwa tukikutana navyo sana ,na hufanyiwa chini ya madaraja nyakati za usiku na kwenye majumba ambayo hayajaisha kujengwa “mapagare”, anasema Kishiwa.
Anasema, hatua ambayo wameichukua ni kuimarisha ulinzi kwenye maeneo yote hatarishi, pamoja na kuwatafuta wazazi wa watoto hao na kuwakabidhi.
Anaongeza kuwa, wanapowarudisha watoto hao kwa wazazi wao, ndani ya siku chache wanawaona tena wakiwa mitaani wakidhurura hovyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga Nasoro Warioba, anasema watoto hao licha ya kulawitiwa pia hufundishwa kulawitiana kwa kuchezeana wenyewe michezo michafu.
Anasema, yeye hua anajenga urafiki na watoto hao, na humueleza kila kitu dhidi ya vitendo vya hudhalilishaji ambavyo hufanyiwa na kufanyiana, na kwamba hatua ambayo huichukua ni kutafuta familia zao na kuwarejesha.
“Watoto hawa wanaishi mazingira mabaya sana mitaani, mimi hua ni rafiki zangu, na nikiwakuta wanavuta gundi za ulevi na wanyang’anya, na hufanyiwa vitendo vya ubakwaji na kulawitiwa hali ni mbaya sana,” anasema Warioba.
Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Mkami Mchango, anasema watoto ambao hufikishwa hospitalini hapo kupata matibabu wakiwa wamebakwa kubakwa na kulawitiwa ni kuanzia umri wa miaka 5 hadi 12.
“Takwimu za mwaka jana, watoto 15 walibakwa na kulawitiwa, wakike 11 na wakiume 4, mwaka huu tumepata watoto watatu, wakike wawili na wakiume mmoja,”amesema Mkami.
Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga Ansila Matheo, anasema wamekuwa wakishirikiana na viongozi wa Serikali za Mitaa, kuwasaka watoto ambao wanaishi mitaani na kisha kuwaunganisha na wazazi wao.
Anasema, mwaka jana wamewaunganisha watoto 27 na wazazi wao, na kwamba zoezi hilo ni endelevu.
“Watoto hawa wanapoishi mitaani, wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya unyanyasaji kingono kwa kubakwa na kulawitiwa, ndiyo maana Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine, tumekuwa tukiwasaka na kuwarudisha kwa wazazi wao,”anasema Ansila.
Meneja Mradi wa Shirika la Reliway Iren Mwampembe, anasema wameanza kufanya kazi Shinyanga kuanzia Mwezi Aprili, kwa kudhibiti wimbi la watoto kuishi mitaani na kuwaunganisha na familia zao, na kwamba tayari wameshakutana na watoto 81.
Anasema, baada ya kukutana na watoto hao, tayari 45 wamesha warudisha kwa wazazi wao, huku watoto 20 ambao bado hawajapata mawasiliano na wazazi wao, wamewahifadhi kwa watu ambao waliwapatia mafunzo ya malezi na makuzi na wataishi nao ndani ya miezi sita tu.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga Victoria Maro, anasema ukatili dhidi ya watoto una sababishwa na wazazi kukosa elimu ya malezi na makuzi dhidi ya watoto, na hali duni ya kifamilia.
Anasema, hatua ambayo wamekuwa wakiichukua, ni kutoa elimu ya malezi na makuzi kwa wazazi dhidi ya watoto wao kwa kuwalea katika misingi bora, pamoja na kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili.
“Jeshi la Polisi dawati la jinsia na watoto, hatua ambayo tunaichukua kudhibiti wimbi la watoto hawa ambao wanaishi mitaani, tumeanza kutoa elimu kwa wazazi ya malezi na makuzi kupitia vikundi vyao, nyumba za Ibada, kaya kwa kaya hasa zile zenye hali duni kimaisha, na kwenye vipindi vya radio za kijamii, na tumefanya zaidi ya mara 10,”anasema Maro.
Anataja takwimu kwamba, ukatili dhidi ya watoto mkoani humo umepungua kwa asilimia 58 tofauti na miaka ya nyuma, ambapo hali ilikuwa mbaya zaidi ya asilimia 90.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS.