Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,237
- 1,744
Zab 121:6 SUV
[6] Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
Kwa Waisraeli kwao jua kali lilihusiana na hatari ya joto kali na upungufu mkubwa wa maji, ukisoma andiko hili ukiwa kwenye nchi au eneo lisilo na jua kali, unaweza usielewe sana. Lakini Waisraeli walielewa sana madhara ya jua.
Na Mwezi ulihusishwa na mambo ya imani, kama vile maradhi mabaya, au hofu za giza, kwao ilikuwa na mashaka mengi wanapoona haya yamekuja kwao. Bila kufahamu mwezi, giza, jua, vilitokana na majira, kwao kulikuwa na maana tofauti kutokana na matukio mabaya yaliyokuwa yanawapata.
Hakikisho la ulinzi wa Mungu kwa waaminio unatolewa hapa, ulinzi wa Mungu usio na kikomo dhidi ya madhara ya asili na ya kiroho ulikuwa wazi kwa wale waliomwamini au kumcha yeye.
Ahadi hii inatuwezesha kufahamu ulinzi wa Mungu ulivyo mkubwa kwetu, anatuhakikishia hata sisi leo, wale wanaomwamini na kumtumaini yeye, wanao ulinzi mkubwa dhidi ya mambo mabaya ya kiroho na kiasili.
Mwamini anayeishi maisha ya kumtegemea Mungu, anao uhakika wa ulinzi wa Mungu masaa 24, hana hofu ya kuvamiwa na adui wa kiroho kuharibu maisha yake, maana anajua anao ulinzi wa uhakika.
Hatari zote za mchana na usiku, Mungu atakulinda nazo, kazi yako ni kuendelea kukaa kwake, kuishi maisha yanayompendeza yeye, utakuwa na ulinzi usio na mipaka katika maisha yako.
Wakati wengine wana mashaka mengi, wana hofu na usalama wa maisha yao kiroho, wana mashaka ya kuvamiwa na wachawi, wana wa Mungu wanaotulivu, wanayo amani, maana wanajua yupo Mungu anayewalinda.
Kwanini usikimbilie kwa Yesu, kwanini usitulie kwa Yesu, ikiwa umeona upo usalama mkubwa namna hii? Hupaswi kuendelea kuishi maisha ya hofu, jikabidhi mbele za Mungu sasa uwe salama.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana