Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Wapendanao ni binadamu kama ambavyo wasiopendana walivyo......nao pia wana mioyo ya nyama na hawawezi kuwa perfect 100%. Kama ambavyo baba huweza kumkosea mwanae, mpenzi pia aweza kumkosea mwenzie.... Kwa mantiki hii walio katika mapenzi nao pia huanguka na kujikuta wanacheat........... Sasa ODM akimmega Eliza, haimaanishi mapenzi yake kwa mama Matesha ndo yameisha. Na ndio maana kama yakitokea haya hufanyika kwa siri kubwa sasa, si hadharani au kumwonyesha mwenzi wake kama ulivyotaka kutuchakachua hapo juu.....Ukisema walitamaniana unakosea Babu sema huyu alimtamani kwa sababu anayefanya unyama huu ni mwenzi mmoja dhidi ya mwingine.
Swali langu sasa kabla hujaondoka na ninaomba jibu la mwisho sitakuuliza tena; ODM anapocheat na Amanda muhudumu wa Bar, au Sophia Secretari wake tunawezasema nakuna penzi la dhati hapo kwa Mama ODM au?
Na unaposema kuwa mwenye kufanya hayo hakuwa na mapenzi ya kweli ina maana inakuwa imekula kwake yeye aliyeolewa/oa mtu wa aina hii lakini akawa na penzi la dhati au haiwezekani mwenye penzi la dhati akakutana na aso penzi la dhati? na je ndoa yenye penzi la aina hii utaiitaje??
Yes, kuna uwezekano mkubwa wa mwenye penzi la kweli akaolewa/oa na aliyemtamani. Hii ni mateso kwa mwenye mapenzi ya kweli. Ukisikia mmoja katika ndoa anataabika kwa manyanyaso na bado anang'ang'ania japokuwa ana uwezo wa kuanza mbele na maisha yake ujue mapenzi hayo ni ya dhati kwa upande mmoja.......... Lakini ukasikia "babue, usinletee za kuleta kama vipi nigaie talaka yangu niende kwetu" afu hata kabla hajamaliza sentensi talaka tatu zishachomekwa kwenye sidiria, ujue hapo hakukuwa na mapenzi ya kweli..... kutamaniana tu.....
Ndoa zenye aina hii ya mmoja mwenye mapenzi ya kweli na mwingine msanii naweza kuziita "ndoa za kifo"..... "mguu ndani mguu nje"
Bado niko hapa kama bado una swali nyoosha kidole juu.