Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Khaaa!Naomba nipingane na wote mlochangia kwenye hii sredi. Mkiona nimekuvunjieni heshima kashtakini kwa Invizibo.
Huu mjadala una mitazamo miwili tofauti kwa maoni yangu na katu hauwezi kuwa sahihi kwa kuuangalia kwa mtazamo mmoja, Penzi linalindwa at the same time Penzi halilindwi (kiswahili kigumu lakini mtanielewa mbele ya safari)
1) PENZI LINALINDWA:
Kumbukeni sisi ni binadamu na tuna madhaifu yetu ambayo kama tukiyapa nafasi kututawala au kuwatawala wenza wetu basi tutakuwa tunalizembea penzi hata kama liwe madhubuti vipi.
Ufafanuzi: Mfano mwanaume ana udhaifu wa tamaa na mwanamke ana udhaifu wa kupenda attention au kupenda kwa mazowea, ni vyema ukamlinda mwenzio ili asiteleze kwa kumwelewesha kukaa mbali na vishawishi ambavyo vinaweza vikapenya kwenye udhaifu wake na kuharibu penzi, haiwezekani mwanamme amruhusu mke wake akalale na marafiki wa kiume eti tu kwasababu anamuamini au mwanamke kumuacha mume wake ajiexpose kwenye vishawishi au mitego ya starehe eti kwasababu tu penzi halilindwi. (Hapa unalinda ili mwenza au wewe mwenyewe usije ukateleza na ukaliathiri pendo na mtiririko wake)
Conclusion: Penzi linalindwa ili lisiingie doa kwa kuzingatia weakness ya mtu/jinsia, mazingira na kwenye wajibu (hapa inaingia kunogesha/kukoleza penzi)
2)PENZI HALILINDWI: hii inabase zaidi kwenye hisia, hisia za mapenzi hazilindwi na wala hazifuatiliwi wala kubadilishwa kirahisi. Yoyote mwenye hisia za mapenzi za kweli anaweza akatawaliwa na tamaa tu lakini moyo utabaki kwa anaempenda na hili halina ubishi. Lakini kumbuka kwamba mtu huyu inabidi alindwe ili asiteleze na akalitia doa pendo, kwa vile mtendwa siku zote hajui moyo wa mtenda kama umebeba penzi la dhati au la usanii, hivyo hata penzi la dhati lina nafasi kubwa ya kuparaganyika kama halijalindwa (refer to Penzi linalindwa, above).
Nimeandika haraka haraka kwavile hapa Igunga internet cafe hawaruhusu ukae zaidi ya dakika 10, hivyo kama hamjanielewe nitakuja kufafanua sku jirani yangu mwenye laptop akilejea holidei.
Nisiulizwe masuali kwa vile sitokuwa hewani.
Kwaherini!
Hapo kwenye bold haiwezi kutokea katika dunia hii!