Ulinzi wa penzi.......

Ulinzi wa penzi.......

Naomba nipingane na wote mlochangia kwenye hii sredi. Mkiona nimekuvunjieni heshima kashtakini kwa Invizibo.

Huu mjadala una mitazamo miwili tofauti kwa maoni yangu na katu hauwezi kuwa sahihi kwa kuuangalia kwa mtazamo mmoja, Penzi linalindwa at the same time Penzi halilindwi (kiswahili kigumu lakini mtanielewa mbele ya safari)

1) PENZI LINALINDWA:
Kumbukeni sisi ni binadamu na tuna madhaifu yetu ambayo kama tukiyapa nafasi kututawala au kuwatawala wenza wetu basi tutakuwa tunalizembea penzi hata kama liwe madhubuti vipi.

Ufafanuzi: Mfano mwanaume ana udhaifu wa tamaa na mwanamke ana udhaifu wa kupenda attention au kupenda kwa mazowea, ni vyema ukamlinda mwenzio ili asiteleze kwa kumwelewesha kukaa mbali na vishawishi ambavyo vinaweza vikapenya kwenye udhaifu wake na kuharibu penzi, haiwezekani mwanamme amruhusu mke wake akalale na marafiki wa kiume eti tu kwasababu anamuamini au mwanamke kumuacha mume wake ajiexpose kwenye vishawishi au mitego ya starehe eti kwasababu tu penzi halilindwi. (Hapa unalinda ili mwenza au wewe mwenyewe usije ukateleza na ukaliathiri pendo na mtiririko wake)

Conclusion: Penzi linalindwa ili lisiingie doa kwa kuzingatia weakness ya mtu/jinsia, mazingira na kwenye wajibu (hapa inaingia kunogesha/kukoleza penzi)

2)PENZI HALILINDWI: hii inabase zaidi kwenye hisia, hisia za mapenzi hazilindwi na wala hazifuatiliwi wala kubadilishwa kirahisi. Yoyote mwenye hisia za mapenzi za kweli anaweza akatawaliwa na tamaa tu lakini moyo utabaki kwa anaempenda na hili halina ubishi. Lakini kumbuka kwamba mtu huyu inabidi alindwe ili asiteleze na akalitia doa pendo, kwa vile mtendwa siku zote hajui moyo wa mtenda kama umebeba penzi la dhati au la usanii, hivyo hata penzi la dhati lina nafasi kubwa ya kuparaganyika kama halijalindwa (refer to Penzi linalindwa, above).

Nimeandika haraka haraka kwavile hapa Igunga internet cafe hawaruhusu ukae zaidi ya dakika 10, hivyo kama hamjanielewe nitakuja kufafanua sku jirani yangu mwenye laptop akilejea holidei.
Nisiulizwe masuali kwa vile sitokuwa hewani.
Kwaherini!
Khaaa!

Hapo kwenye bold haiwezi kutokea katika dunia hii!
 
pesa ni sabuni ya roho bhana,fanya vyooote lakin kama huna talanta mfukoni mambo hayaendi katika ilo penzi,nawasiisha
 
Penzi haliwezi kulindwa(kibinadamu) ila linaboreshwa...penzi ni hisia ya mtu juu ya mtu mwingine...sasa utalindaje hisia ya mtu? kitu kisichoonekana kwa macho ya nyama...hisia zimekaa kiroho zaidi...unless na wewe uko kiroho pia..PENZI linaboreshwa ktk kukumbushana/kutimiza(kupalilia) wajibu...ila kiroho unaweza kulinda..hebu niishie hapa.

hapa nakubaliana na ww mia. Kama anataka kukusaliti atakusaliti tu. Haijalishi yupo wapi,na nani muda gani n.k
 
Penzi la kweli halipo utegemeana na nyakati ukaribu na mazingira....... ulinzi pekee wa penzi ni ukaribu wenu tofauti na hapo tegemea Dhoruba kali
 
Shida imeletwa na usasa/kukua lugha!? kuwa wajibu(amri) ktk ndoa umegeuzwa kuwa ni favor(ulinzi?)...ndugu zangu mke kumhudumia mme ni wajibu na atahesabiwa haki ktk hilo..kadhalika mme kumtunza mke ni wajibu naye atahesabiwa...wajibu umegeuka kulinda sasa...wajibu (amri) ni torati iliyoandikwa ktk mioyo yetu bila kujali unaamini nini..usipotunza mke/me,watoto tayari umehukumiwa.. ndo hizo tunazosikia laana ya mke/me/wtt haiangalii jinsia, dini au rangi ni kichapo tu. Tunachanganya ulinzi na wajibu..
 
Back
Top Bottom