Ulinzi wa Rais Samia umebadilishwa?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Tangu akiwa ziara ya Arusha alipokutana na wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki na sasa yupo mkoani Mbeya, nimegundua kama ulinzi umebadilika kiaina.

Zamani tulizoea kuona jammer car katika msafara wa Rais lakini kwasasa gari lile halionekani kabisa.

Pia wale jamaa zetu wenye silaha nzito ambapo kipindi cha awamu ya 5 kuna waliosema wanatokea kwa "tolu" siku hizi hawapi tena kwenye msafara wa mama.

Je kuna mabadiliko katika ulinzi wa Rais Samia?
 
Alaf walinzi wenye hizi sare kipindi cha magu watu walisema wanatoka nje ya nchi 😀😀
Kweli watu wanapigana na mtu ambaye hawamjui
 
Katiba mbele Mungu nyuma.
😂uwe kwnye mfumo usiomtaka Mungu then umlete Mungu.
Mungu ana Serikali yake na yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…