Ulinzi wa wananchi dhidi ya polisi ni jukumu la nani?

Ulinzi wa wananchi dhidi ya polisi ni jukumu la nani?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Ni wimbo tunaoimbiwa kila siku kuwa usalama wa raia na mali zao ni jukumu la polisi. Kuhusu hili lina ukweli kiasi gani, hasa katika mazingira yetu ya sasa, huo ni mjadala mwingine. Leo nitajielekeza kwenye swali la msingi, ulinzi wa wananchi dhidi ya polisi ni jukumu la nani?

Dhana ya ulinzi wa wananchi kuwa ni jukumu polisi, bila shaka inafanya kazi katika nadharia kuwa kila askari ataandaliwa kwa weredi mkubwa katika misingi uzalendo na uadilifu kuwa malaika mlinzi wa kutumainiwa na wananchi. Katika dhana hii, polisi panategemewa kuwa ni sehemu ambapo mtu yeyote anapokabiliwa na tishio angekimbilia kusalimisha maisha yake. Tathmini ya kama hivi ndivyo haswa ilivyo taswila ya jeshi la polisi kwa wananchi ni jambo linalohitaji utafiti wa peke yake, hivyo sitalizungumzia.

Hoja yangu itakuwa ni swali la dhahania, Je, ikiwa baadhi ya polisi wataasi majukumu yao, badala yake wakaamua kutumia upolisi wao kuvunja sheria kuwaonea wananchi, kuna mifumo gani thabiti ya kuwalinda wananchi dhidi ya polisi wa namna hii?

Wasi wasi wangu ni kuwa mwananchi anapigwa na polisi, halafu anaambiwa aende akashtaki polisi, kuna uhakika gani kuwa polisi watamtendea haki? Haya ni maswali magumu yanayofikirisha sana.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujifanya hayapo. Kama tunaamini kuwa polisi wetu ni watu na kwamba wanaweza kughafilika katika utekelezaji wa viapo vyao, ni vyema kama jamii tukaanza kufikiria kujenga mifumo ya kujilinda dhidi yao, mathalani uimarishaji wa mifumo ya haki jinai na haki za binadamu.
 

Attachments

  • IMG-20250623-WA0005.jpg
    IMG-20250623-WA0005.jpg
    123.3 KB · Views: 22
ni vyema kama jamii tukaanza kufikiria kujenga mifumo ya kujilinda dhidi yao, mathalani uimarishaji wa mifumo ya haki jinai na haki za binadamu
Hili ndio la msingi kwa sasa, ukitegemea Police akusaidie ujue umeisha. YAANI ni Sawa na kumuomba au kumtegemea Mamba akuvushe kwenye mto!
 
Wananchi wakianza battle na polisi, wananchi watashinda.
 
Ni wimbo tunaoimbiwa kila siku kuwa usalama wa raia na mali zao ni jukumu la polisi. Kuhusu hili lina ukweli kiasi gani, hasa katika mazingira yetu ya sasa, huo ni mjadala mwingine. Leo nitajielekeza kwenye swali la msingi, ulinzi wa wananchi dhidi ya polisi ni jukumu la nani?

Dhana ya ulinzi wa wananchi kuwa ni jukumu polisi bila shaka inafanya kazi katika nadharia kuwa kila askari ataandaliwa kwa weredi mkubwa katika misingi uzalendo na uadilifu kuwa malaika mlinzi wa kutumainiwa na wananchi. Katika dhana hii, polisi panategemewa kuwa ni sehemu ambapo mtu yeyote anapokabiliwa na tishio angekimbilia kusalimisha maisha yake.

Tathmini ya kama hivi ndivyo haswa ilivyo taswila ya jeshi la polisi ilivyo kwa wananchi ni jambo linalohitaji utafiti wa peke yake, hivyo sitalizungumzia.

Hoja yangu itakuwa ni swali la dhahania, Je, ikiwa baadhi ya polisi wakiasi majukumu yao, badala yake wakaamua kutumia upolisi wao kuvunja sheria kuwaonea wananchi, kuna mifumo gani thabiti ya kuwalinda wananchi dhidi ya polisi wa namna hii?

Wasi wasi wangu ni kuwa mwananchi anapigwa na polisi, halafu anaambiwa aende akashtaki polisi, kuna uhakika gani kuwa polisi watamtendea haki? Haya ni maswali magumu yanayofikirisha sana.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujifanya hayapo.

Kama tunaamini kuwa polisi wetu ni watu na kwamba wanaweza kughafilika katika utekelezaji wa viapo vyao, ni vyema kama jamii tukaanza kufikiria kujenga mifumo ya kujilinda dhidi yao, mathalani uimarishaji wa mifumo ya haki jinai na haki za binadamu.
Mtu wakwanza kabisa ni wmananchi mwenyewe, unawajibika kwa ulinzi wako binafsi
 
Sasa hivi imekuwa ni vigumu kutofautisha kati ya polisi na jambazi.
 
Back
Top Bottom