Ulipataje kiwanja chako?

Mimi nilinunua kiwanja mwaka 2008 kwa bei ya sh mil 1.5,nakumbuka nilitafutiwa kazi nikawa nalipwa elf 50 kwa mwezi nikataka niikatae ila mama akanipa moyo nikaifanye,lakin huwez amini marupu rupu niliyokuwa nakutana nayo kwenye hyo kazi yakanifanya ninunue kiwanja na kujenga nyumba ya room 3,
 
Unadhani wale waliobomolewa Kimara walikuwa hawauliziani Kama unavyosema.

Njia ya kuuliza Jirani sio ya kuamini sana
 
Aisee hongera sana kwa bahati hio. Na pia hongera kwa kujenga.
 
Yes na ndiyo maana kwenye post yangu hapo juu nimekazia sana kuuuliza majirani, hao ndiyo watatoa status ya ukweli juu hicho kiwanja na kama kina shida ni lazima watakuambia tu pasipo kupepesa macho
 
Dalali, muuzaji, mtendaji, balozi hawa huwa ni kitu kimoja wote wanaangalia ulaji, ila jirani ndiyo mtu wa mwisho
 
Unadhani wale waliobomolewa Kimara walikuwa hawauliziani Kama unavyosema.

Njia ya kuuliza Jirani sio ya kuamini sana
Sasa mambo ya kubomolewa inatokea hata majirani pia wanaweza wasijui, ila akishawailizia majirani akaombe kibali cha ujenzi building permit ili apate kuambiwa panafaa au hapafai
 
Wangapi wamejenga maeneo salama lakini bado serikali wakipataka panavunjwa
Mara nyingi serikali inakulipa na kupewa kiwanja kilicho pimwa, si unaona Kipawa? walipewa viwanja vilivyopimwa Chanika. na unalipwa kulingana na eneo lako kwa mfano km palipimwa na afisa Ardhi na serikali ikapataka tena Pesa yake ni kubwa zaidi plus thamani ya jengo. kuliko aliye jenga sehemu ya kiholela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…